Headlines News :
Home » » MAJAMBAZI YAMPORA SH. MILIONI 12, MKIONGOZI WA KUNDI LA MUZIKI ARUSHA

MAJAMBAZI YAMPORA SH. MILIONI 12, MKIONGOZI WA KUNDI LA MUZIKI ARUSHA

Written By Bashir Nkoromo on Monday, June 25, 2012 | 10:07 AM

Na Rose Jackson, ARUSHA,TANZANIA
MSIMAMIZI wa kundi la muziki la Contagious lenye makazi yake jijini Arusha,Njara Rasolomanana maarufu kama Dady amevamiwa na kundi la majambazi nyumbani kwake Kimandulo jijini hapa ambapo alijeruhiwa na kisha  kuporwa vitu mbalimbali vyevye  thamani ya kiasi cha zaidi ya
sh,12 milioni.
    Tukio hilo lilitokea mwishoni mwa wiki iliyopita majira ya saa 1.30 asubuhi ambapo  kundi la majambazi 17 wakitumia jiwe aina ya fatuma walivunja mlango wake na kisha kumjeruhi kabla ya kumpora vitu mbalimbali.
   Akihojiwa na gazeti hili huku akionyesha majeraha katika eneo la uso na mgongo ke,Rasolomanana alisema kwamba wezi hao walifanikiwa kumpora simu tano,kompyuta ndogo tatu,na kiasi cha sh,4 milioni.
   Njara ,ambaye ni raia wa Madagascar alisema kwamba tayari ameshafungua jalada la tukio hilo katika kituo kikuu cha polisi cha kati jijini Arusha na kupewa nambari za AR|RB|7548|2012 .
    Kamanda mkuu wa jeshi la polisi mkoani Arusha,Liberatus Sabas alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kwamba jeshi lake bado linafuatilia kwa kina tukio hilo kwa lengo la kuwashikilia watuhumiwa.
Share this article :

0 comments:

Speak up your mind

Tell us what you're thinking... !

Total Pageviews

Comments

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. theNkoromo SPORTS - All Rights Reserved
Template Design by Creating Website Published by Mas Template