Headlines News :
Home » » YANGA YAICHANA AFRICAN LYON 4-0

YANGA YAICHANA AFRICAN LYON 4-0

Written By Bashir Nkoromo on Monday, August 20, 2012 | 12:05 PM

Yanga wakishangilia

Timu ya Yanga imeibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Africfan Lyon, zote za Dar es Salaam katika mchezo wa kirafiki wa kujipima nguvu uliofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Yanga ilitumia mchezo huo kuwapima wachezaji wake kabla ya kuanza kwa Ligi Kuu na haukuwa mwanzo mbaya, timu ikicheza kwa utulivu na hata kuhimili vishindo vya wapinzani.

Didier Kavumbangu, mshambuliaji mpya wa klabu hiyo aliyesajiliwa kutoka Atletico Olympique ya Burundi, alikuwa wa kwanza kuwainua vitini mashabiki wa Yanga dakika ya sita baada ya kupiga mpira ambao beki alipojaribu kuokoa ulimgonga kipa wake na kuingia nyavuni.Hadi mapumziko, Yanga walikuwa mbele kwa bao hilo 1-0.

Kipindi cha pili, Haruna Niyonzima aliifungia Yanga bao la pili kwa penalti dakika ya 57, baada ya Simon Msuva kuchezewa rafu na Semmy Kessy kwenye eneo la hatari
Frank Damayo aliyeingia kuchukua nafasi ya Athumani Iddi ‘Chuji’ kipindi cha pili alitoa pasi nzuri kwa Simon Msuva ambaye aliifungia Yanga bao la tatu dakika ya 72, kabla ya Jerry Tegete kufunga la nne dakika ya 90+1.

Baada ya mchezo huu, Yanga ambao ni mabingwa wa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame inatarajiwa kuondoka Dar es Salaam Jumatano kwenda Kigali, Rwanda ambako itaweka kambi ya wiki mbili kujiandaa na Ligi Kuu.

Ikiwa huko, Yanga itacheza mechi kadhaa za kujipima nguvu na vigogo wa Rwanda, kama APR, Rayon, Atracao na Polisi kabla ya kurejea Dar ves Salaam kuanza maandalizi ya Ligi Kuu. Chanzo: Bin Zubery Blog  kupitia Liwazo Zoto Blog
Share this article :

0 comments:

Speak up your mind

Tell us what you're thinking... !

Total Pageviews

Comments

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. theNkoromo SPORTS - All Rights Reserved
Template Design by Creating Website Published by Mas Template