Headlines News :
Home » » BONDIA MASHALI KUPAMBANA NA MGANDA

BONDIA MASHALI KUPAMBANA NA MGANDA

Written By Bashir Nkoromo on Wednesday, September 19, 2012 | 5:09 AM


DAE ES SALAAM, TANZANIA
Bondia wa Ngumi za kulipwa nchini Thomas Mashali (pichani), amesaini mkataba wa kucheza pambano la ubingwa wa Afrika Mashariki na Kati na Bondia Medi Sebyala wa Uganda mchezo utakaofanyika Oktoba 14 mwaka huu katika Ukumbi wa friends Corner.

Akizungumza na waandishi wa habari Mratibu wa mpambano huo unaosimamiwa na Shirikisho la Ngumi za kulipwa TPBO Regina Gwae amesema leo kwamba mpambano huo ni maandalizi ya kuhakikisha bondia Thomas mashali sasa anavuka mipaka ya Tanzania baada ya kufanya vyema nchini.

“huwezi kwenda nje kama ndani hufanyi vizuri na huwezi kwenda ulaya Afrika mashariki ukaikimbia hivyo tumeona tumpe mchezo Afika mashjariki ili akifanya vyema aweze kuvuka mipaka hiyo sasa, alisema Regina.

Amesema kwa upandewa mazungumzo na Bondia Medi Sebyala yamekamilika na tayari ameshatumiwa Mkataba wake kwa ajili ya pambano hilo.

“ pamabano hilo litakuwa na raundi 10 na watacheza katika uzito wa kilo 72 na kama tujuavyo ukizungumzia mabondia wa uzito wa kati wanaotamba nchini na afrika mashariki kwa ujumla huwezi kuacha kuwataja mashali na sebyala,alisema regina.

Regina amesema tunataraji mpambano utakuwa mzuri wenye kuvutia kwa kuwa Mashali ni bondia mzuri na Sebyala nae ni Bondia Mzuri aliyeweka historia ya kuwasumbua mabondia Fransis Cheka wa Morogoro na rashidi Matumla kwa nyakati Tofauti.

Pia amewaomba wafadhili kujitokeza kudhamini mchezo huo unatarajiwa kuwa na mapambanio yaq utangulizi yenye kuvutia ambapo mabondia wake waktatangazwa baadae watakaosindikiza mpambano huo.
Share this article :

0 comments:

Speak up your mind

Tell us what you're thinking... !

Google+ Followers

Total Pageviews

Comments

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. theNkoromo Blog: SPORTS PAGE - All Rights Reserved
Template Design by Creating Website Published by Mas Template