Headlines News :
Home » » BONDIA RAJABU MAOJA AENDA KUZIPIGA NAMIBIA

BONDIA RAJABU MAOJA AENDA KUZIPIGA NAMIBIA

Written By Bashir Nkoromo on Thursday, September 27, 2012 | 9:03 AM

*Anakwenda kwenye programu ya “IBF Utalii wa Michezo”
*Kunyukana na bingwa wa Namibia mpambano wa IBF Africa.
 NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM, TANZANIA
Mtanzania Rajabu mtoto wa Jumanne Maoja mkazi wa jiji la Tanga anaondoka na Shirika la Ndege la Afrika ya Kusini (South African Airways) kuelekea jijini Windhoek, Namibia ambako ana kibarua kikali kuiwakilisha Tanzania kwenye IBF Utalii wa Michezo (IBF Sports Tourism).

Taarifa ya Kamisheni ya ngumi za kulipwa  Tanzania (TPBC) imesema, Maoja atakutana na bingwa wa nchi ya Namibia, Goettlieb Ndokosho kwenye mpambano uliopewa jina la “Vita Vya Jangwa la Kalahari” (The Battle for the Kalahari Desert) na waandaaji wa mpambano huo wa raundi 12 kumpata bingwa wa IBF Afrika katika uzito wa unyoya. Kinda Boxing Promotions inayoongozwa na bwana Simon Nangolo ambaye ni mkaguzi mwandamizi wa ndani wa mahesabu (Senior Internal Auditor) nchini Namibia ndio waandaaji wa mpambano huo wakukata na shoka.

Kwa mujibu wa TPBC, mshindi wa mpambano huo atakutana na bingwa wa IBF Afrika, Mashariki ya Kati, Ghuba ya Uarabu na Uajemi, Mtanzania Ramadhani Shauri ambaye hivi karibuni alimkung’uta bondia Sande Kizito wa Uganda katika mpambano ulioishia raundi ya 8 baada ya Kizito kushindwa kuendelea.

"Huu unakuwa mpambano wa tatu kwa Watanzania mwaka huu kuwania ubingwa wa IBF katika bara la Afrika, Mashariki ya Kati ya Ghuba ya Uajemi ambako tayari mikanda miwili ya IBF iko Tanzania", imesema taarifa hiyo.

Taarifa imeongeza kwamba, mpambano wa Mtanzania Rajabu Jumanne Maoja na Goettlieb Ndokosho wa Namibia utafanyika katika jiji la Windhoek, mji mkuu wa nchi ya Namibia tarehe 29 Septemba siku ya Jumamosi na kwamba Maoja atafuatana na Kocha wake Ibrahim Raphael Jorum ambaye naye anatoka katika jiji la Tanga.

Msimamizi mkuu wa mpambano huo ni Mtanzania Onesmo Alfred McBride Ngowi ambaye atalisimamia pambano hilo lililo na upinzania mkubwa!
Share this article :

0 comments:

Speak up your mind

Tell us what you're thinking... !

Total Pageviews

Comments

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. theNkoromo SPORTS - All Rights Reserved
Template Design by Creating Website Published by Mas Template