Headlines News :
Home » » KILIMANJARO PREMIUM LAGER YAZIPA SIMBA NA YANGA MABASI YA KIFAHARI

KILIMANJARO PREMIUM LAGER YAZIPA SIMBA NA YANGA MABASI YA KIFAHARI

Written By Bashir Nkoromo on Friday, September 21, 2012 | 5:46 AM

 Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia Bia yake Kilimanjaro Premium Lager, leo imezikabidhi mabasi mapyaa ya kisasa aina ya Yutong, kila timu basi moja ambayo yote ghama yake ni sh. milioni  450. Pichani, Makamu Mwenyekiti wa Yanga  Clement Sanga (kushoto) na Mwenyekiti wa Simba, Aden Rage wakipongezana baada ya kukabidhiwa mabasi hayo, Makao Makuu ya TBL jijini Dar es Salaam. Katikati yao ni Mkurugenzi Mtendaji wa TBL, Robin Goetzsche. Wengine ni viongozi wa timu hizo na viongozi wa TBL.
 Mwanzoni mwa hafla hiyo, ni Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF)  Angetile Oseah akijadiliana jambo na waandishi wa habari, Majuto Omari (kushoto) na Efraim Kibonde, makao makuu ya TBL ilala jijini Dar es Salaam.
 Mabasi ya kifahari aina ya Yutong yakiwa makao makuu ya TBL kusubiri makabidhiano
 Mashabiki wa Simba wakiingia na matarumbeta makao makuu ya TBL kwenye makabidhiano ya mabasi hayo
 Mashabiki wa Yanga vilevile nao wakiingia na matarumbeta makao makuu ya TBL kwenye makabidhiano ya mabasi hayo
 Kisha wakakutana na kuanza kuserebuka pamoja, lakini wakitupiana maneno, vijembe na tambo kwa nyimbo.
 Shabiki wa Simba akimtania mwenzake wa Yanga kwa kumuonyesha tatu bila...
 Mwenyekiti wa Simba Aden Rage, akiserebuka na shabiki wa Yanga wakati wa hafla hiyo.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Executive Solutions ambayo inasimamia udhamini wa Kilimanjaro Premium Lager kwa Simba na  Yangay na Taifa Stars , Aggrey Marealle  akizungumza wakati wa hafla hiyo
 Meneja wa bia ya Kilimanjaro Premium Lager, George Kavishe akizungumza wakati wa hafla hiyo
 Shabiki wa Simba akiwatambia wa Yanga
 Shabiki wa Yanga akimtambia Rage aliyeketo meza kuu
 Makamu Mwenyekiti wa Yanga Clement Sanga akibadilishana hati na Mkurugenzi Mkuu wa TBL Robin Goetzsche
 Mkurigenzi Mtendaji Robin Goetzsche akibadilishana hati na Mwenyekiti wa Simba Aden Rage
 Stephen Kilindo wa TBL akizungumza wakati wa hafla hiyo
 Rage akikabidhiwa mfano wa ufunguo wa basi na Mkurugenzi Mtendaji wa TBL
 Sanga akikabidhiwa mfano wa ufunguo wa gari na Mkurugenzi Mtendaji wa TBL
 Viongozi na mashabiki wa timu za Yanga na Simba wakiwa mbele ya mabasi hayo wakati wa makabidhiano
 Mtaalam kutoka kampuni ya ASAK Enterprises Edward Mongela akimuonyesha dereva wa Yanga Martin Mtui, jinsi ya ku-opareti baadhi ya vitu kwenye basi walilokabidhiwa Yanga
 Dereva wa Simba Mohamed Kigomba ndanbi ya basi jipyaaaa la Simba
 Mwenyekiti wa Simba Aden Rage akimshikia mpira Makamu Mwenyekiti wa Yanga Clement Sanga wakati akitia sainbi yake kwenye mpira. Katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa TBL. Robin Goetzsche
Bosi katika TBL akipeperusha bendera kuruhusu mabasi yaanze kuondoka Makao makuu ya TBL ambapo yalitembezwa kupitia mitaa mbalimbali na kwenye baadhi ya matawi ya Yanga na ya Simba na kisha kupelekwa makao makuu ya timu hizo. (Picha zote na Bashir Nkoromo)
Share this article :

0 comments:

Speak up your mind

Tell us what you're thinking... !

Google+ Followers

Total Pageviews

Comments

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. theNkoromo Blog: SPORTS PAGE - All Rights Reserved
Template Design by Creating Website Published by Mas Template