Headlines News :
Home » » SIMBA KUANZA RAUNDI YA NANE KWA KAGERA SUGAR

SIMBA KUANZA RAUNDI YA NANE KWA KAGERA SUGAR

Written By Bashir Nkoromo on Tuesday, October 16, 2012 | 9:34 AM


NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM
Ligi Kuu ya Vodacom kuwania ubingwa wa Tanzania Bara inaingia raundi nane kesho (Oktoba 17 mwaka huu) kwa mechi tano huku vinara wa ligi hiyo Simba wakiialika Kagera Sugar kutoka mkoani Kagera kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Mechi hiyo namba 52 itachezeshwa na mwamuzi Ronald Swai kutoka Arusha wakati waamuzi wasaidizi ni Julius Kasitu na Methusela Musebula, wote kutoka Shinyanga. Mwamuzi wa akiba ni Ephrony Ndisa wa Dar es Salaam huku mtathimini wa waamuzi akiwa Charles Mchau kutoka Moshi.

Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya utakuwa mwenyeji wa mechi kati ya Tanzania Prisons inayofundishwa na Jumanne Chale na Azam iliyo chini ya kocha Boris Bunjak kutoka Serbia. Nayo Polisi Morogoro iliyopanda msimu huu itakuwa mwenyeji wa JKT Ruvu kwenye Uwanja wa Jamhuri.

Mgambo Shooting ambayo imepata ushindi mara mbili mfululizo itakuwa nyumbani Uwanja wa Mkwakwani, jijini Tanga ikiikaribisha Toto Africans katika mechi itakayochezeshwa na Geofrey Tumaini wa Dar es Salaam. Oljoro JKT inayonolewa na Mbwana Makata itakuwa nyumbani Uwanja wa Kumbukumbu ya Sheikh Kaluta Amri Abeid jijini Arusha dhidi ya African Lyon.
Share this article :

0 comments:

Speak up your mind

Tell us what you're thinking... !

Total Pageviews

Comments

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. theNkoromo SPORTS - All Rights Reserved
Template Design by Creating Website Published by Mas Template