Headlines News :
Home » » TAARIFA MUHIMU KWA WANACHAMA WA TFF

TAARIFA MUHIMU KWA WANACHAMA WA TFF

Written By Bashir Nkoromo on Tuesday, October 16, 2012 | 10:07 AM


Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ilikutana Oktoba 11, 2012 kujadili michakato ya chaguzi mbalimbali za wanachama wa Shirikisho. Katika kikao chake, Kamati ilijadili michakato ya chaguzi za viongozi wa Chama cha Mpira wa Miguu cha Mkoa wa Rukwa (RUREFA), Chama cha Waamuzi wa Mpira wa Miguu (FRAT), Chama cha Mpira wa Miguu cha Mkoa wa Shinyanga (SHIREFA) na Chama cha Mpira wa Miguu cha Mkoa wa Dar es salaam (DRFA),.
Pia Kamati ilijadili mchakato wa chaguzi za Chama cha Madaktari wa Michezo (TASMA) na kupokea mchakato wa Chama cha Mpira wa Miguu cha Mkoa wa Mbeya (MRFA).
Baada ya kujadili chaguzi hizo kwa kina, Kamati ilifikia uamuzi ufuatao:
1.       FRAT
Uchaguzi wa FRAT haukufanyika baada ya wajumbe kugoma wakipinga kuondolewa kwa baadhi ya wagombea. Kamati ilikubaliana kuiagiza Kamati ya Uchaguzi ya FRAT kuhakikisha uchaguzi unafanyika Novemba 17, 2012 na kufanya maandalizi yote muhimu ikiwa ni pamoja na sehemu ambako uchaguzi huo utafanyika. Mkutano utatakiwa kuwapigia kura wajumbe waliopitishwa kugombea uongozi tu.

2.       RUREFA
Baada ya kufuta uchaguzi wa viongozi wa RUREFA na kuivunja Kamati ya Uchaguzi ya RUREFA, Kamati ya Uchaguzi ya TFF imeitaka Kamati ya Utendaji ya RUREFA kuteua kamati mpya ya uchaguzi ya chama hicho kabla ya Oktoba 20, 2012 na kuiagiza kamati mpya kuwa imeshatangaza mchakato wa uchaguzi ifikapo Oktoba 24, 2012.

3.       SHIREFA
Kamati ilipokea pingamizi dhidi ya baadhi ya wagombea uongozi wa SHIREFA na hivyo kuagiza walioweka pingamizi na waliowekewa pingamizi pamoja na mwakilishi wa Kamati ya Uchaguzi ya SHIREFA kuhudhuria kikao cha Kamati ya Uchaguzi ya TFF kitakachofanyika Alhamisi ya Oktoba 18, 2012 kwa ajili ya maamuzi ya mwisho.

4.       MRFA
Kamati ilipokea rufaa na pingamizi kutoka kwa baadhi ya wagombea walioenguliwa kuwania uongozi wa chama hicho na hivyo imewataka walioweka pingamizi na waliokata rufaa kuhudhuria kikao cha Kamati ya Uchaguzi ya TFF kitakachofanyika Oktoba 18, 2012 jijini Dar es salaam.

5.       TASMA
Kamati iliona mapungufu katika mchakato wa uchaguzi wa viongozi wa TASMA na kuamua chama hicho kifanye uchaguzi ifikapo Desemba mosi badala ya uchaguzi kufanyika  Oktoba 27, 2012 kama ilivyokuwa imepangwa awali. Kamati ya Uchaguzi ya TFF inaiagiza Kamati ya Uchaguzi ya TASMA kuhakikisha kasoro zilizojitokeza zinarekebishwa ili uchaguzi ufanyike kwa mujibu wa Katiba ya chama hicho na Kanuni za Uchaguzi.

6.       DRFA
Awali, Kamati ya Uchaguzi ya TFF ilitangaza kuwa hatma ya uchaguzi wa DRFA itajulikana baada ya kikao cha leo, lakini kutokana na wajumbe kutoweza kuhudhuria kwa sababu tofauti, mustakabali wa suala hilo sasa utajulikana baada ya kikao cha Oktoba 18, 2012.

Wagombea na wadau wanaotakiwa kuhudhuria kikao cha Oktoba 18, 2012 wanataarifiwa kuwa kikao hicho kitafanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa ofisi za TFF kuanzia saa 08:2012.
Kamati inawaomba wajumbe wote kuhudhuria bila ya kukosa. 

Angetile Osiah
Katibu Mkuu TFF
Share this article :

0 comments:

Speak up your mind

Tell us what you're thinking... !

Total Pageviews

Comments

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. theNkoromo SPORTS - All Rights Reserved
Template Design by Creating Website Published by Mas Template