Headlines News :
Home » » CHEKA NA CHIMWEMWE KUKUTANA TENA ADDIS ABABA, ETHIOPIA KATIKA PAMBANO LA MARUDIANO

CHEKA NA CHIMWEMWE KUKUTANA TENA ADDIS ABABA, ETHIOPIA KATIKA PAMBANO LA MARUDIANO

Written By Bashir Nkoromo on Tuesday, December 18, 2012 | 7:06 AM


DAR ES SALAAM, Tanzania
Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Nchini (TPBC) tayari imemtafutia bondia Francis Cheka mpambano wa marudiano kati yake na bondia Chiotra Chimwemwe wa Malawi katika jiji la Addis Ababa, Ehtiopia.

Mpambano huo utafayika January 26, siku ya ufunguzi wa mkutano wa wakuu wa nchi za Africa (AU Summit) katika jiji hilo la Wafalme la Abesinia!

Cheka na Chimwemwe watakutana jijini Arusha Desemba 26 (Boxing Day) katika mpambano wa kutafuta nani mbabe wa uzito wa Super Middle katika bara la Afrika, Mashariki ya Kati na Ghuba ya Uajemi (IBF AMEPG). Katika mpambano huo mafahali hawa wawili wataumana kiume kwa raundi 12 za dakika tatu kila mmoja!

Mpambano wa Cheka na Chimwemwe jijini Arusha umeandaliwa na kampuni ya Screen Hills (T) Investment ya jijini Dar-Es-Salaam inayomilikiwa na promota maarufu aliyewahi kuwa bingwa wa taifa katika ngumi za ridhaa na kulipwa Andrew George aka Chagga Boy!

Umaarufu wa wawili hawa umewafanya mapromota wanaoandaa tamasha la kuchangisha pesa kwa ajili ya kulisha watu wenye njaa katika bara la Africa kuwaingiza Cheka 26(15)-6(3)-1 na Chiotra 26(15)-4(2)-1 katika mpambano hwa marudiano utakaofanyika jijini Addis Ababa, Ethiopia tarehe 26 Januaru 2012!

Katika tamasha hilo, pambano kuu litakuwa kati ya bondia Oliver McCall 56(37)-12(1)-0 kutoka Marekani ambaye aliwahi kuwa bingwa wa uzito wa juu duniani akipambana na bondia Sammy Retta - 18(17)-3(2)-0 kutoka Ethiopia kugombea ubingwa wa IBF Africa, Mashariki ya Kati na Ghuba ya Uajemi (IBF AMEPG) katika uzito wa juu (Heavyweight)

Mapambano mengine yatawakutanisha mabondia Daniel Wanyonyi 14(12)-5(2)-2 wa Kenya atakayechuana na bondia Issac Hlatswayo 30(10)-5(3)-1 kutoka Afrika ya Kusini katika kugombea ubingwa wa IBF Afrika, Mashariki ya Kati na Ghuba ya Uajemi (IBF AMEPG) katika uzito wa Welterweight

Naye Manzur Ali 7(4)-8(3)-0 bingwa wa uzito wa juu kutoka nchi ya Misri atachuana vikali na bondia Harry Simon 27(20)-0-0 kutoka Namibia ubingwa wa IBF Afrika, Mashariki ya Kati na Ghuba ya Uajemi (IBF AMEPG) katika uzito wa Light heavyweight.

Mpambano huu umeidhinishwa na Shirikisho la Ngumi la Kimataifa (IBF) na Cheka kupewa kibali na Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Nchini (TPBC).

Imetolewa na: Onesmo A,M, Ngowi, Rais, TPBC na Rais, IBF /Africa
Share this article :

0 comments:

Speak up your mind

Tell us what you're thinking... !

Total Pageviews

Comments

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. theNkoromo SPORTS - All Rights Reserved
Template Design by Creating Website Published by Mas Template