Headlines News :
Home » » KILIMANJARO STARS KUCHEZA NUSU FAINALI ALHAMISI

KILIMANJARO STARS KUCHEZA NUSU FAINALI ALHAMISI

Written By Bashir Nkoromo on Tuesday, December 4, 2012 | 5:57 AM


DAR ES SALAAM, TANZANIA
Timu ya Tanzania Bara (Kilimanjaro Stars) itacheza nusu fainali ya michuano ya Kombe la Chalenji 2012 Alhamisi (Desemba 6 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Mandela ulioko Namboole jijini Kampala, Uganda.

Kilimanjaro Stars ambayo itacheza mechi hiyo na mshindi wa robo fainali ya kesho (Desemba 4 mwaka huu) kati ya wenyeji Uganda na Ethiopia imeingia hatua hiyo baada ya kuitoa Rwanda. Mechi imechezwa leo (Desemba 3 mwaka huu) Uwanja wa KCC ulioko Lugogo, Kampala.

Mabao ya Amri Kiemba dakika ya 33 na John Bocco dakika ya 53 ndiyo yaliyoifanya Kilimanjaro Stars itinge nusu fainali na kuifungisha virago Rwanda (Amavubi) inayofundishwa na Milutin ‘Micho’ Sredojovic kutoka Serbia.

Vijana wa Kilimanjaro Stars wanaonolewa na Kim Poulsen walitawala pambano hilo, hasa kipindi cha kwanza kwa pasi fupi fupi. Kilimanjaro Stars imefungwa bao moja katika mechi nne ilizocheza tangu michuano hiyo ilipoanza Novemba 24 mwaka huu jijini Kampala.

Kilimanjaro Stars ambayo katika michuano hiyo iliyofanyika Dar es Salaam mwaka jana iliishia hatua ya nusu fainali iliwakilishwa na; Juma Kaseja, Erasto Nyoni, Amir Maftah, Shomari Kapombe, Kelvin Yondani, Amri Kiemba, Salum Abubakar/Athuman Idd, Frank Domayo, Mwinyi Kazimoto, John Bocco na Mrisho Ngasa.

MICHUANO YA KOMBE LA UHAI KUANZA DESEMBA 7
Michuano ya Kombe la Uhai inayoshirikisha timu za U20 za klabu za Ligi Kuu ya Vodacom inatarajia kuanza Desemba 7 mwaka huu na kumalizika Desemba 22 mwaka huu.

Wachezaji watakaoshiriki michuano hiyo ni wale tu ambao usajili wao umefanyika Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na kupata leseni. Hakutakuwa na usajili mwingine wowote mbali na ule uliofanyika sambamba na wa Ligi Kuu.

Taratibu zote za michuano hiyo zitafahamishwa kwa klabu husika ikiwemo ratiba ya michuano hiyo.

Share this article :

0 comments:

Speak up your mind

Tell us what you're thinking... !

Total Pageviews

Comments

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. theNkoromo SPORTS - All Rights Reserved
Template Design by Creating Website Published by Mas Template