Headlines News :
Home » » MWINJUMA, SONYO KURINDIMA MTWARA

MWINJUMA, SONYO KURINDIMA MTWARA

Written By Bashir Nkoromo on Thursday, January 24, 2013 | 5:12 AM


MTWARA, Tanzania
Victoria Band ya jijini Dar es Salaam chini ya Mwinjuma Muumini leo inatarajiwa kufanya onyesho la nguvu  katika ukumbi wa Klabu ya Bandari mjini hapa.

Bendi hiyo iliyoweka kambi ya mazowezi mjini hapa baada ya kusukwa upya na wanamuziki wapya kutoka bendi kubwa hapa nchini itaonyesha kazi iliyofanyika katika maficho hayo ya takribani mwezi mmoja na nusu tangu mwishoni mwa mwaka jana,

“Tunaibuka mafichoni na vibao vpya vya moto vine ambavyo wapenzi wa Mtwara kutokana na ukarimu wao wa kulienzi kambi yetu leo watapata fursa ya kuwa mashuhuda wa kwanza wa kazi hiyo” Alisema Mwinjuma katika mahojiano na mwandishi wa habari hizi kambini kwa.

Kwa mujibu wa Mwin-juma onyesho hilo   litaviipua jikoni  vibao vyake vinne vya nyimbo mpya zilizopikwa na kuiva  kwenye chungu hicho ambavyo anaamini vitatoa ushuhuda wa kazi ya kambi hiyo.

Alizitaja  nyimbo hizo anazoamini kuwa zitazima kiu ya wapenzi wa muziki wa dansi nchini kuwa  ni pamoja na Shamba la bibi na Utafiti wa mapenzi zilizotungwa na yeye mwenyewe.

Zingine ni Mama Bahati uliyotungwa  mpiga rizim Yohana Mbatizaji wakati  Sonyo atakiipua kibao chake cha Mwisho wa siku.

Kesho watafanya mjini Lindi wakiwa njiani kurudi Dar es Salaam na baada wiki moja ya mapumziko kundi hilo lenye makao makuu yake Mbagala Kiburugwa  litaingia studio kurekodi nyimbo zake mpya saba.

Mwin juma na Waziri Sonyo wakizungumzia kambi hiyo walisema imepata mafanikoyo makubwa ambayo hawakutarajiwa kwa kuvipika na kuivisha vibao hivyo na kingine kikiwa kinatokota vingine viwili vinaandaliwa kupikwa.

Walidai mafanikiyo hayo yalitokana na kuwa mafichoni ambako umakini, utulivu na dhamira ya  ilichowaleta Mtwara ilitawala pamoja na kuridhishwa na huduma ya kambi iliyowawezesha kufanya mazowezi kwa saa nane kila siku isipokuwa Ijumaa tu.

Muumini alisema kazi iliyofanyika ni nzito na wapenzi wa muziki wasubiri burudani ya nguvu na kutamba kuwa wapinzani wao kimuziki watakuwa ni Twanga na FM Academia tu kwa kilinganisha na kiwango cha
juu kilichofikiwa na bendi hiyo Bandi hiyo iliyoanzishwa karibu miaka saba iliyopita Mbagala Kiburugwa
jijini Dar es Salaam iliundwa tena kwa kusukwa upya na kundi la wanamuzi wenye vipaji katika idara mbalimbali kutoka bendi maarufu hapa nchini.

Miongoni mwa wanamuziki hao wapatao 24 ni pamoja na Rais wa Bendi Muumini Mwinjuma Kiongozi wao Sellemani Mumba ambae ni mpiga solo na mpiga kinanda Moshi Hamisi kutoka Twangapepeta.

Wengine ni mpiga bass gita George Gama ambaye ni Katibu pamoja na Mshauri wa Bendi ambaye pia  mtunzi na mwimbaji Waziri Sonyo.

Waimbaji wengine ni Januari Joseph a.k Eleven,binti Ciana Jodan, mtoto Max Bushoke Ramso Bushoke, Jonas Mlembuka na Rapa wao Mussa Kalenga.

Wengine waliyokuwa katika kambi hili lililoanza Desemba 15 mwaka jana ndani ya majengo ya SabaSaba Chikongola mjini hapa na baadae kuhamia Ligula B. Mpiga Bass Kassimu Mumba, Drum Abdala Hussein Kinanda Moshi Hamisi na Tumba Vaninga Swalehe.

Timu hiyo inakamilishwa na madansa wao wanaopikwa na Bokilo Omari Mussa Kutoka TOT, ni Joha Juma,Mariam Othaman Farida Omari, Lilian Wayanga, Nadia Benjamin  na Sophia Ramadhani.

Onyesho litasindikizwa na wazee wa kazi wa kanda hii ya kusini band ya Bandari wana Boka Boma wakongwe wa muziki wa dansi katika mikoa hii ya kusini ya Mtwara na Lindi hawana mpinzi wanasema usijaribu.
Share this article :

0 comments:

Speak up your mind

Tell us what you're thinking... !

Total Pageviews

Comments

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. theNkoromo SPORTS - All Rights Reserved
Template Design by Creating Website Published by Mas Template