Headlines News :
Home » » UCHAGUZI WA VIONGOZI WA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF) NA TANZANIA PREMIER LEAGUE BOARD (TPL BOARD) 04/02/2013

UCHAGUZI WA VIONGOZI WA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF) NA TANZANIA PREMIER LEAGUE BOARD (TPL BOARD) 04/02/2013

Written By Bashir Nkoromo on Monday, February 4, 2013 | 8:24 AM


DAR ES SALAAM, Tanzania
Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) inawataarifu wananchi wote kwamba baada ya kufanya usaili kwa waombaji uongozi wa TFF  na Tanzania Premier League Board (TPL Board), Kamati imefanya maamuzi yafuatayo:

1.       TANZANIA PREMIER LEAGUE BOARD

(a)                 Waombaji uongozi wafuatao wamekidhi matakwa ya Kanuni za uendeshaji za TPL Board na Kanuni za Uchaguzi za TFF. Kamati inawatangaza kuwa wagombea wa nafasi walizoomba kama ilivyoonyeshwa hapa chini:

NAFASI INAYOGOMBEWA
S/N0.
JINA
MWENYEKITI WA TPL BOARD
1.
Hamad Yahya Juma
2.
Yusufali Manji


MAKAMU MWENYEKITI WA TPL BOARD
1.
Said Muhammad Said Abeid (Kupitishwa kwake kutategemea matokeo ya uhakiki wa vyeti vyake)
MJUMBE –KAMATI YA UENDESHAJI (Management  Committee)

1.

Kazimoto Miraji Muzo

2.
Omary Khatibu Mwindadi

(b)                Mwombaji uongozi Ndg. Christopher Peter Lunkombe hakukidhi matakwa ya Kanuni za uendeshaji za TPL Board  Ibara ya 28(2)  kwa kuwa cheti chake cha Elimu ya Sekondari kina utata. Kamati ya Uchaguzi ya TFF imemwondoa kugombea nafasi ya Mjumbe wa Kamati ya uendeshaji (Management Committee) ya TPL Board.

2.       SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

(a)     Waombaji uongozi wafuatao wamekidhi matakwa ya Katiba ya TFF na Kanuni za Uchaguzi za TFF. Kamati inawatangaza kuwa wagombea wa nafasi walizoomba kama ilivyoonyeshwa hapa chini:

NAFASI
S/No.
JINA
RAIS WA TFF
1.
Athumani Jumanne Nyamlani
2.
Jamal Emily Malinzi

MAKAMU WA RAIS WA TFF


2.
Ramadhan Omar Nassib           
3.
Wallace Karia
MJUMBE WA KAMATI YA
UTENDAJI –
Kanda ya 1 (Kagera, Geita)

           
1.
Kalilo Samson
2.
Salum Hamis Umande Chama


Kanda ya 2 (Mwanza, Mara)
1.
Jumbe Oddessa Magati
2.
Mugisha Galibona
3.
Samwel Nyalla
4.
Vedastus F.K Lufano


Kanda ya 3 (Shinyanga, Simiyu)
1.
Epaphra Swai



Kanda ya 4 (Arusha, Manyara)


1.
Elley Simon Mbise
2.
Omar Walii Ali  


Kanda ya 5 (Tabora, Kigoma)
1.
Ahmed Idd Mgoyi
2.
Yusuf Hamis Kitumbo


Kanda ya 6 (Rukwa, Katavi)


1.
Blassy Mghube Kiondo
2.
Seleman Bandiho Kameya (Kupitishwa kwake kutategemea matokeo ya uhakiki wa vyeti vyake)


Kanda ya 7 (Iringa, Mbeya)
1.
David Samson Lugenge
2.
John Exavery M. Kiteve
3.
Lusekelo E. Mwanjala


Kanda ya 8 (Ruvuma, Njombe)
1.
James Patrick Mhagama
2.
Stanley W. D Lugenge


Kanda ya 9 (Mtwara, Lindi)
1.
Athuman Kingome Kambi
2.
Francis Kumba Ndulane
3.
Zafarani Mzee Damoder


Kanda ya 10 (Dodoma,  Singida)
1.
Hussein Zuberi Mwamba
2.
Stewart Ernest Masima


Kanda ya 11 (Morogoro, Pwani)


1.
Riziki Juma Majala
2.
Twahil Twaha Njoki


Kanda ya 12 (Kilimanjaro, Tanga)
1.
Davis Elisa Mosha
2.
Khalid Abdallah Mohamed
3.
Kusianga Mohamed Kiata


Kanda ya 13 (Dar es salaam)
1.
Alex Crispine Kamuzelya
2.
Juma Abbas Pinto
3.
Muhsin Said Balhabou   


(b)    Waombaji uongozi wafuatao hawakukidhi matakwa ya Katiba ya TFF na Kanuni za Uchaguzi za TFF. Kamati ya Uchaguzi ya TFF imewaondoa kugombea nafasi walizoomba kama ilivyoonyeshwa hapa chini:

(i)                   Ndg. Omary Mussa Nkwarulo anayeonba kugombea nafasi ya Rais wa TFF hakukidhi matakwa ya Katiba ya TFF na  Kanuni za Uchaguzi za TFF Ibara ya 9(7) kwa kutokuwa na ufahamu wa kuridhisha kuhusu majukumu na wajibu wa nafasi anayoomba na uwezo wa kutekeleza majukumu na malengo ya TFF.

(ii)                 Ndg. Michael Richard Wambura anayeonba kugombea nafasi ya Makamu wa Rais wa TFFhakukidhi matakwa ya Katiba ya TFF na  Kanuni za Uchaguzi za TFF ibara ya 9(7) kuwa Ndg. Michael Wambura alifungua kesi ya madai namba 100 ya 2010 kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es salaam dhidi ya Mwenyekiti wa Klabu ya Simba akiwa ni mwanachama wa Klabu ya Simba, kinyume na Katiba ya Klabu ya Simba. Kwa kufanya hivyo, Ndg. Michael Wambura alivunja Katiba ya Klabu ya Simba, alikiuka Katiba ya TFF na Katiba ya FIFA.

(iii)                Pia Kamati inaheshimu maamuzi yaliyotolewa na Kamati ya Rufaa ya TFF kuhusu uchaguzi mwaka 2008 kwamba Bw. Michael R. Wambura hakukidhi matakwa ya Ibara ya 29(7) ya Katiba ya TFF na Ibara ya 9 ya Kanuni za Uchaguzi za TFF. Kwa mujibu wa  Katiba ya TFF na Kanuni za Uchaguzi za TFF, Kamati  ya Uchaguzi ya TFF haina mamlaka ya kubadilisha maamuzi yaliyofikiwa na Kamati hiyo ya Rufaa. Maamuzi hayo yanaweza tu kubadilishwa na Mahakama ya usuluhishi wa masuala ya michezo (CAS).  

(iv)               Ndg. Abdallah Hussein Musa anayeomba kugombea nafasi ya Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Kupitia Kanda Na. 1 (Kagera, Geita) hakukidhi matakwa ya Katiba ya TFF na  Kanuni za Uchaguzi za TFF ibara ya 9(7) kwa kutokuwa na ufahamu wa kuridhisha kuhusu majukumu na wajibu wa nafasi anayoomba na uwezo wa kutekeleza majukumu na malengo ya TFF.

(v)                 Ndg.  Mbasha Matutu anayeomba kugombea nafasi ya Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Kupitia Kanda Na. 3 (Shinyanga, Simiyu)  hakukidhi matakwa ya Katiba ya TFF na  Kanuni za Uchaguzi za TFF ibara ya 9(7) kwa kuwa aliingilia mchakato wa Uchaguzi kwa kushirikiana na waweka pingamizi dhidi ya mgombea mwenzake.

(vi)               Ndg. Charles Mugondo anayeomba kugombea nafasi ya Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Kupitia Kanda Na. 4 (Arusha, Manyara) hakukidhi matakwa ya Katiba ya TFF na  Kanuni za Uchaguzi za TFF  kwa kuwa vyeti vyake vya Elimu ya Sekondari na cheti cha Ualimu vina utata.

(vii)              Ndg. Ayubu Nyaulingo anayeomba kugombea nafasi ya Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Kupitia Kanda Na.  6 (Rukwa, Katavi) hakukidhi matakwa ya Katiba ya TFF na  Kanuni za Uchaguzi za TFF ibara ya 3  inayotaka awe na uzoefu wa uendeshaji wa Mpira wa Miguu uliothibitishwa wa angalau miaka mitano (5) na pia  hakukidhi Ibara ya 9(7) kwa kutokuwa na ufahamu wa kuridhisha kuhusu majukumu na wajibu wa nafasi anayoomba na uwezo wa kutekeleza majukumu na malengo ya TFF.

(viii)            Ndg. Nazarius A.M Kilungeja anayeomba kugombea nafasi ya Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Kupitia Kanda Na.  6 (Rukwa, Katavi) hakukidhi matakwa ya Katiba ya TFF na  Kanuni za Uchaguzi za TFF ibara ya 9(7) kwa kuwa amekuwa sehemu ya migogoro ya muda mrefu mkoani Rukwa.

(ix)               Ndg. Eliud Peter Mvella anayeomba kugombea nafasi ya Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Kupitia Kanda Na.  7 (Iringa, Mbeya) hakukidhi matakwa ya Katiba ya TFF na  Kanuni za Uchaguzi za TFF ibara ya 9(7) kwa kuwa si mwaminifu kwa kukiuka uamuzi wa pamoja wa Kamati ya Utendaji ya TFF  kuhusu mabadiliko ya Katiba.

(x)                 Ndg. Farid Nahdi anayeomba kugombea nafasi ya Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Kupitia Kanda Na. 11 (Morogoro, Pwani) hakukidhi matakwa ya Katiba ya TFF na  Kanuni za Uchaguzi za TFF ibara ya 9(2) na (7) kwa kuwa maelezo ya umri wake na  vyeti vya elimu havikubaliani.

(xi)               Ndg. Hassan Othuman Hassan anayeomba kugombea nafasi ya Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Kupitia Kanda Na. 11 (Morogoro, Pwani) hakukidhi matakwa ya Kanuni za Uchaguzi za TFF ibara ya 11(5) kwa kuwa  hakuhudhuria usaili.

(xii)              Ndg. Omary Isack Abdulkadir anayeomba kugombea nafasi ya Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Kupitia Kanda Na. 13 (Dar es salaam) hakukidhi matakwa ya Kanuni za Uchaguzi za TFF ibara ya 9(7) kwa kuwa  alikaidi maagizo ya TFF ya kuahirisha uchaguzi wa chama cha Waamuzi wa Mpira wa Miguu Tanzania  (FRAT) na maagizo ya TFF kwa kuwa alienguliwa kwenye mchakato wa uchaguzi wa FRAT kwa kutotimiza matakwa ya Kanuni za uchaguzi za wanachama wa TFF.

(xiii)            Ndg. Shafii Kajuna Dauda anayeomba kugombea nafasi ya Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Kupitia Kanda Na. 13 (Dar es salaam) hakukidhi matakwa ya Kanuni za Uchaguzi za TFF ibara ya 9(7) kwa kuwa si mkweli: aliposhindwa kwenye uchaguzi wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es salaam (DRFA) alipotosha umma kuhusu ushiriki wake kwenye uchaguzi huo na mchakato mzima wa uchaguzi. Pia hana ufahamu kuhusu Katiba ya TFF na majukumu ya Kamati ya Utendaji ya TFF. 

3.       Usaili uliofanyika kwa waombaji uongozi ulizingatia pia taarifa zilizoifikia Kamati ya Uchaguzi ya TFF kupitia pingamizi zilizowasilishwa dhidi ya waombaji uongozi wa TFF na TPL Board.

4.       Uchaguzi wa TPL Board utafanyika tarehe 22 Februari 2013, na Uchaguzi wa TFF utafanyika tarehe 24 Februari 2013 jijini Dar es salaam.


Deogratias Lyatto
MWENYEKITI
KAMATI YA UCHAGUZI TFF
Share this article :

0 comments:

Speak up your mind

Tell us what you're thinking... !

Total Pageviews

Comments

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. theNkoromo SPORTS - All Rights Reserved
Template Design by Creating Website Published by Mas Template