Headlines News :
Home » » KABURU NAYE AACHIA NGAZI SIMBA

KABURU NAYE AACHIA NGAZI SIMBA

Written By Bashir Nkoromo on Thursday, March 7, 2013 | 9:51 AM


MAMBO ndani ya klabu ya Simba yamezidi kuwa hovyo baada ya Makamu Mwenyekiti wa klabu hiyo, Geofrey Nyange 'Kaburu'  naye kutangaza kujiuzulu.

Kaburu anakuwa kiongozi wa pili wa klabu hiyo kwa leo kuachia ngazi ambapo aliyefungua milango alikuwa Mjumbe wa kamati ya Utendaji na Mwenyekiti wa kamati ya Usajili, Zacharia Hanspoppe.

Viongozi hao wamefikia hatua hiyo baada ya kutoridhishwa na mwenendo mzima wa klabu hiyo ambayo hivi karibuni imekuwa ikifanya vibaya kwenye michezo yake ya ligi kuu soka Tanzania Bara, kabla ya kutolewa kwenye ligi ya Mabingwa Afrika na Recreativo do Libolo ya Angola kwa jumla ya mabao 5-0.

Habari zilizopatikana jino hii zinaeleza kwamba Kaburu ameiwasilisha barua ya kujiuzulu kwake kwa njia ya barua pepe kwa Mwenyekiti wa klabu hiyo, Alhajj Ismail Aden Rage ambaye kwa sasa yupo nchini India akitibiwa mgongo.

Aidha, Poppe naye amewasilisha barua yake ya kujiuzulu kwake kwa Katibu Mkuu wa timu hiyo, Evodius Mtawala ambaye amethibitisha kupokea barua hiyo na kusema pia amepokea barua pepe ya Kaburu.IMETAYARISHWA NA DINA ISMAIL BLOG
Share this article :

0 comments:

Speak up your mind

Tell us what you're thinking... !

Google+ Followers

Total Pageviews

Comments

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. theNkoromo Blog: SPORTS PAGE - All Rights Reserved
Template Design by Creating Website Published by Mas Template