Home »
» BIGRIGHT AMREJESHA KASEBA ULINGONI
BIGRIGHT AMREJESHA KASEBA ULINGONI
Bondia Jafet Kaseba anategemea kupanda tena ulingoni mwanzoni mwa mwezi wa sita kuzipiga na bondia toka kenya joseph magudha katika mpambano wa kimataifa. hivyo maandalizi yamekwishaanza kwa kuwaanda mabondia watakaocheza utangulizi,kwa kuweka mapambano makali likiwemo la kamanda wa makamanda atakaezipiga na ibrahim maokola. mwanzoni maokola alikuwa amepangwa azipige na bondia toka moro na kamanda kupewa bondia mwingine, lakini kulitokea kupishana kwa maneno kati ya mabondia hao kiasi cha kutaka kupigana kavu, mabondia na viongozi waliokuwepo hapo akiwemo ibrahim kamwe walipendekeza ibadilishwe wapinzani na wawili hao wazipige kukata ngebe na majigambo ya ubabe waliyokuwa wakitupiana.mpaka sasa mapambano ya utangulizi inategemea kuwa juma seleman atazipiga na issa omar,juma fundi atapigana na moro best, yohana mathayo atazipiga joseph onyango toka kenya. na mapambano mengine yatajulishwa hapo baadae zoezi la usainishaji mikataba likikamilika
| bingwa wa kike na msaidizi wa promota pendo njau akisimamia zoezi la usainishaji wa mikataba ya mabondia,likiwemo pambano la kuondoa utata kati ya kamanda na maokola,.bigright jafet kaseba na mabondia wengi walishuhudia. |
| bondia kamandawamakanda kushoto akitunishiana misuli na ibrahim maokola baada ya kusaini pambano lao.JPG
367K View Share Download |
0 comments:
Speak up your mind
Tell us what you're thinking... !