Headlines News :
Home » » TBL YAHIMIZA POOL KUENEZWA MIKOA YOTE TANZANIA BARA

TBL YAHIMIZA POOL KUENEZWA MIKOA YOTE TANZANIA BARA

Written By Bashir Nkoromo on Thursday, May 2, 2013 | 7:01 AM


VYAMA vya mchezo wa pool kuanzia wilaya hadi taifa vimetakiwa kutumia vizuri udhamini wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kuhakikisha mchezo huo unaenea katika mikoa yote ya Tanzania Bara.

Hayo yalisemwa jana na diwani wa kata ya Kitanzini katika Manispaa ya Iringa, Jesca Msambatavangu wakati alipokuwa mgeni rasmi wakati wa kukabidhi vifaa vya michezo kwa vyuo vikuu vitakavyoshiriki mashindano ya mchezo huo kwa wanafunzi wa elimu ya juu ngazi ya mkoa wa Iringa ya 'Higher Learning Pool Competition 2013'.

Msambatavangu alisema kuwa ni vema vyama vya mchezo huo vikatumia nafasi ya udhamini huo vizuri katika kuhakikisha mchezo wa pool unapanuka zaidi ili hatimaye uchezwe kila mkoa kwa mikoa yote ya Tanzania Bara kuanzia kwenye klabu na vyuo vikuu.

"Nitakuwa mchoyo wa fadhila kama sitawashukuru na kuwapongeza TBL kupitia bia ya Safari Lager kwa kuutoa mbali mchezo wa pool na hatimaye kuufikisha hapa ulipo na pia udhamini wa kampuni yenu si katika mchezo wa pool pekee bali ni mambo mengi mnayoyafanya kwenye jamii katika kuchangia maendeleo ya taifa letu na serikali inalitambua hilo,"alisema Msambatavangu.

Aliongeza kwa kuwataka vijana wengi kuendelea kujitokeza kujifunza kucheza mchezo huo ambao kwa sasa ni ajira kwa vijana wanaoucheza.

Katika kile kilichoonekana kuwa ni mmoja wa wadau wa mchezo huo, diwani huyo aliahidi kutoa mbuzi mmoja mmoja kwa kila chuo kinachoshiriki mashindano hayo.

Naye mwenyekiti wa chama cha mchezo huo mkoa wa Iringa (IRPA), Salim Kisaku alisema kuwa mashindano hayo yatakayoshirikisha vyuo vikuu vinne yatafanyika kesho kwenye ukumbi wa Twisters Club.

Kisaku alivitaja vyuo vitakavyoshiriki mashindano hayo kuwa ni Ruaha, CDTI, Mkwawa na Tumaini.
Alisema kuwa chuo kitakachobeba ubingwa wa mkoa huo ndiyo kitakachoushirikisha katika fainali za taifa za mashindano hayo zitakazofanyika juni mosi jijini Dar es Salaam.

Meneja wa Kampuni ya TBL mkoani hapa, Josephat Changwe alisema kuwa bingwa wa mashindano hayo kwa upande wa timu katika mkoa huo atajinyakulia fedha taslim Sh.500,000, mshindi wa pili Sh.300,000, mshindi wa tatu Sh.200,000 na mshindi wa nne Sh.100,000.

Changwe alisema kuwa kwa upande wa mchezaji mmoja mmoja (wanaume) bingwa atazawadiwa Sh.150,000 na mshindi wa pili Sh.100,000 wakati kwa upande wa wanawake bingwa atapewa Sh.100,000 na mshindi wa pili Sh.50,000.

Meneja wa Kampuni ya Bia Tanzania(TBL) Mkoa wa Iringa, Josephat Changwe (kushoto) akimkabidhi tisheti Diwani wa Kata ya Kitanzini Manispaa ya Iringa Mjini, Jesca Msambatavangu ili awakabidhi vyuo shirika vya elimu ya juu kwenye mashindano ya Pool kwa vyuo hivyo Iringa jana.Kulia ni Mwenyekiti wa chama cha Pool Mkoa wa Iringa Salum Kisaku.
4
Diwani wa Kata ya Kitanzini Manispaa ya Iringa Mjini, Jesca Msambatavangu(wa pili kushoto) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa hafla fupi ya kukabidhi vifaa vya michezo kwa vyo shiriki vya mashindano ya Pool yanayotarajiwa kuanza kesho Mkoa wa Iringa.Kushoto ni Meneja wa Kampuni ya Bia Tanzania(TBL) Mkoa wa Iringa, Josephat Changwe.Kutoka kulia ni Katibu wa chama cha pool Mkoa wa Iringa,Haji Kiyeyeu na Mwenyekiti wa chama hicho,Salum Kisaku.
1.JPGDiwani wa Kata ya Kitanzini Manispaa ya Iringa Mjini, Jesca Msambatavangu (kushoto) akimkabidhi tisheti nahodha wa timu ya chuo Kikuu cha Ruaha, Said Mohamed wakati wa hafla fupi ya kukabidhi vifaa vya michezo kwa vyuo shiriki vya mashindano ya Pool kwa Vyuo vya Elimu ya Juu Mkoa wa Iringa.Katikati Kushoto ni Mwenyekiti wa Chama cha Pool Mkoa wa Iringa,Salumu Kisaku na Katibu wa chama hicho,Haji Kiyeyeu.
View   Share   Download  
Share this article :

0 comments:

Speak up your mind

Tell us what you're thinking... !

Total Pageviews

Comments

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. theNkoromo SPORTS - All Rights Reserved
Template Design by Creating Website Published by Mas Template