Headlines News :
Home » » BINTOU YAWA SCHMILL A.K.A "THE VOICE" BONDIA WA KIKE MWAFRIKA NCHINI UJERUMANI

BINTOU YAWA SCHMILL A.K.A "THE VOICE" BONDIA WA KIKE MWAFRIKA NCHINI UJERUMANI

Written By Bashir Nkoromo on Saturday, June 8, 2013 | 11:48 PM

Unapozungumzia mchezo wa ngumi au ndondi nchini ujerumani Jina la Bondia wa kike mwafrika BINTOU YAWA SCHMILL A.K.A "THE VOICE" (PICHANI) ndiye anayemudu uringo "Boxing Ring" na kulipeperusha bara la Afrika ughaibuni.

Bondia  huyo kike  Bintou Yawa Schmill mwenye maskani kule Drackenburg nje kidogo ya mji wa Bremen,amekuwa kivutio kwa washabiki wa kimataifa na tishio kwa wapinzani wake anapokuwapo
ulingoni.

Boxer Bintou Yawa Schmill mzaliwa wa Togo mwenye makao yake nchini ujerumani alianza kucheza ngumi akiwa na umri mdogo na kushinda mara 14 katika mashindan 24 na mara 4 K.O ,katoka draw mara 2 uzito wa Water weight 63.5 Kg, katika ngumi za ridhaa.

Kuanzia mwaka 2007 Boxer Bintou Yawa Schmill  a.k.a "The Voice" alihamua kucheza kungumi za kulipwa kwa uzito wa Water weight 64.0 Kg, mwenye urefu mita 1.70 amepigana na kushinda professional Record 4 na Ushindi wa K.O mara 3.

Boxer Bintou Schmill kwa sasa kajiandaa kupambambana na bondia yeyote yule wa kike na mahala popote  duniani.
PICHA ZAIDI ZA BONDIA HUYO



Share this article :

0 comments:

Speak up your mind

Tell us what you're thinking... !

Total Pageviews

Comments

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. theNkoromo SPORTS - All Rights Reserved
Template Design by Creating Website Published by Mas Template