Bingwa Mtetezi wa Kikombe cha Mkombozi Kitayosce FC atafungua michuano hiyo kwa kucheza na Green Star zote za mjini Moshi Mkoani Kilimanjaro.
Kwa mujibu wa ratiba ya Mkombozi Cup michuano hiyo itaendeshwa kwa makundi, ambapo kundi A lina Bingwa Mtetezi Kitayosce FC, Green Star, Nyuki FC na Golani FC.
Mechi ya Ufunguzi imepangwa kuchezwa Juni 13 mwaka huu katika uwanja wa Mandela, Kata ya Pasua Mjini Moshi.
Kundi B lina Kili Rangers, Mvuleni, Nazareth na Soweto. Kundi C lina TPC, New Generation FC, Best Maridadi FC na Moshi UTD. Kundi D limeundwa na Reli, Sango Kili FC na Boys United
Katika kutangaza makundi hayo klabu ya Machava FC NA Polisi Kilimanjaro hazitashiriki.
Pia vifaa kwa ajili ya mashindano hayo vimtolewa kwa timu zote ikiwemo mipira na jezi.
Mwenyekiti wa Mashindano haya Mama Mshana amewataka wadau wa soka wilayani Moshi kujitokeza kwa wingi kushuhudia michuano ya kuinua vipaji wilayani humu.
Mkombozi Cup itatia nanga Julai 8 mwaka huu, na viwanja vya King George Memorial na Mandela vitatumika, kwa timu 16 kuchuana vikali kumpata Bingwa wa Mkombozi Cup 2013. PICHA;BOFYA AHAPA
MAKUNDI YA MKOMBOZI CUP 2013 KATIKA JEDWALI
MKOMBOZI CUP 2013
| ||||
KUNDI A
|
KUNDI B
|
KUNDI C
|
KUNDI D
| |
1
|
KITAYOSCE
|
KILI RANGERS
|
TPC
|
RELI
|
2
|
GREEN STAR
|
MVULENI
|
NEW GENERATION
|
SANGO
|
3
|
NYUKI FC
|
NAZARETI
|
BEST MARIDADI
|
KILI FC
|
4
|
GOLANI FC
|
SOWETO FC
|
MOSHI UTP
|
BOYS UTD
|
0 comments:
Speak up your mind
Tell us what you're thinking... !