Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Safari Lager, leo imetangaza rasmi kudhamini mwa mara nyingine mashindano ya taifa ya mchezo wa Pool kwa mwaka huu ("Safari Lager National Pool Championships 2013). Pichani, Meneja wa bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo akizindua mashindano hayo, baada ya kutangaza udhamini, katika ukumbi wa Safari Pub, Makao Makuu ya TBL jijini, Dar es Salaam. Kushoto ni Katibu wa Chama Cha mchezo wa Pool Tanzania (TAPA) Amos Kafyinga na kulia ni Mwenyekiti wa waamuzi wa mchezo huo nchini, Hashim Shaweji.
Mwenyekiti wa waamuzi wa mchezo huo nchini, Hashim Shaweji, akizungumza katika hafla ya TBL kutangaza udhamini huo, leo kwenye ukumbi wa Safari Pub, Makao Makuu ya TBL jijini Dar es Salaam. Wapili Kushoto ni Meneja wa bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo aliyetangaza udhamini huo, na kulia ni Katibu wa Chama Cha mchezo wa Pool Tanzania (TAPA) Amos Kafyinga
Home »
» TBL YATANGAZA UDHAMINI WA SAFARI LAGER NATIONAL POOL CHAMPIONSHIPS 2013
0 comments:
Speak up your mind
Tell us what you're thinking... !