Headlines News :
Home » » SHIWATA WAWAFAGILIA JK, OBAMA KWA KUPENDA SPOTI

SHIWATA WAWAFAGILIA JK, OBAMA KWA KUPENDA SPOTI

Written By Bashir Nkoromo on Wednesday, July 3, 2013 | 5:26 AM

MTANDAO wa Wasanii Tanzania (SHIWATA) umempongeza Rais wa Marekani,
Barack Obama na mwenyeji wake Rais Jakaya Kikwete kutambua mchango wa
wasanii, wachezaji wa mpira hasa pale walipocheza ngoma na mpira wa
miguu na mpira wa kikapu.

Mwenyekiti wa Mtandao wa Wasanii Tanzania (SHIWATA), Caasim Taalib
alisema jana kuwa kitendo cha Rais Obama na mwenyeji wake Rais Kikwete
kucheza ngoma za asili alipowasili kwenye uwanja wa Ndege wa Kimataifa
wa Mwalimu Nyerere (DIA) imeonesha namna ambavyo wanaguswa na
utamaduni wa mtanzania.

Alisema pia kuwa hatua ya Rais Obama kutambua mchango wa mtanzania,
Hasheem Thabit anayecheza mpira wa kikapu ligi ya NBA nchini Marekani
kunaimanish anatambua Tanzania ilivyojaliwa na vipaji ndiyo maana
mchezaji huyo amekuwa nyota kati ya waliosajiliwa kuchezea timu za
ligi hiyo.

Taalib alisema ni faraja kubwa kuona Rais Obama kuonesha ufundi wake
kumiliki mpira kwa kichwa na kumpasia Rais Kikwete alipotembelea
mitambo ya kufua umeme ya Symbion ambayo ni mshirika wa Klabu ya
Sunderland.

‘SHIWATA baada ya kujua mchango wa Rais Obama iliahirisha Tamasha la
Mastaa Chipukizi lililokuwa lifanyike Jumamosi Juni 29 kijiji cha
wasanii Mwanzega Mkuranga ili kutoa nafasi kwa  wasanii na viongozi
mbalimbali kushiriki kikamilifu katika maandalizi na mapokezi ya  Rais
Obama’

SHIWATA ambayo inaundwa na wasanii, wanamichezo, wanahabari na vijana
wapatao 7,000 iliahirisha tamasha hilo na sasa litafanyika Agosti
mwaka huu ambapo itakabidhi nyumba kwa mchezaji wa zamani wa Timu ya
Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’, Jellah Mtagwa na wasanii wengine 14
ambao wamekamilisha michango ya ujenzi  wa nyumba zao katika kijiji
chao cha Mwanzega Kimbili, Mkuranga.

Wengine watakaokabidhiwa nyumba zao ni msanii maarufu nchini, Lumole
Matovola ‘Big’ wa Bongo movie ambaye ni mwanachama wa SHIWATA wangine
ni Mwandishi wa Habari, Josephine Moshi, Farida Ndimbo wa Jeshi la
Magereza, Flora Kafwembe wa JKT Mgulani na Nyanza Kisadugwa wa Jeshi
la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).

 Mpaka sasa SHIWATA imejenga nyumba 24 kwa ajili ya wasanii katika
eneo la hekari 300 na wanajiandaa kulima shamba la hekari 500
walizonazo ili kujikwamua kimaisha.
Share this article :

0 comments:

Speak up your mind

Tell us what you're thinking... !

Total Pageviews

Comments

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. theNkoromo SPORTS - All Rights Reserved
Template Design by Creating Website Published by Mas Template