Headlines News :
Home » » SIMBA KUADHIMKISHA SIKU YAO JUMAMOSI, AGOSTI 10, 2013

SIMBA KUADHIMKISHA SIKU YAO JUMAMOSI, AGOSTI 10, 2013

Written By Bashir Nkoromo on Friday, August 9, 2013 | 12:09 PM

 Klabu ya Soka ya Simba, Jumamosi hii ya tarehe 10 Agosti, 2013, itaadhimisha siku yake, 'Simba Day' katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Utaratibu wa kuwa na Simba Day ulianzishwa na klabu hiyo kwa lengo la kuwa na siku ambapo wapenzi, wanachama, viongozi, wachezaji wa zamani na wa sasa pamoja na watu wengine mashuhuri, hukutana kwa pamoja na kusherehekea klabu ambayo imewafanya wawe wamoja pamoja na tofauti nyingi walizonazo.

Mwaka huu, shughuli hiyo itafanyika katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. 

Pamoja na mambo mengine, Simba SC inatarajiwa kucheza mechi ya kirafiki na klabu ya soka ya Sports Club Villa kutoka nchini Uganda.

Katika kusherehesha tukio hilo, wasanii maarufu kama vile Juma Nature, Tunda Man na Snura maarufu kwa jina la ‘Mama Majanga’ watatumbuiza uwanjani hapo.
Share this article :

0 comments:

Speak up your mind

Tell us what you're thinking... !

Google+ Followers

Total Pageviews

Comments

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. theNkoromo Blog: SPORTS PAGE - All Rights Reserved
Template Design by Creating Website Published by Mas Template