TIMU ya Soka ya Villa Squad Fc ya Magomeni Kinondoni, Jijni Dar es Salaam inayoshiriki michuano ya Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara (FDL), imewaangukia wadau wa soka kuipiga tafu ili kuweza kurejea ligi kuu Tanzania Bara.
Akizungumza leo mweka hazina wa timu hiyo, Alwan Geyash alisema kuwa hadi sasa klabu hiyo inaukata mkubwa hali inayopelekea kuvunjika nguvu hata hivyo wanawaomba wadau kujitokeza na kuichangia kufikia malengo yake kwani wanaamini ikiwezeshwa itaweza kurejea ligu kuu.
“Timu ina uwezo na molali wa kutosha, lakini mifuko imekauka kiasi tunachopata cha kuchangishana viongozi wenyewe kwa wenyewe ni kidogo, tunaomba wadau wa soka kujitokeza na kutuchangia kuongeza nguvu zaidi ya kufanya vizuri” alisema Alwan.
Na kuongeza kuwa, kwa wadau watakao guswa wanaweza kufika katika klabu hiyo iliyopo Magomeni Mtaa wa Kionga ama kuchangia kupitia akaunti ya benki ya DTB namba 0704757001 (villa squad football club)au kupitia tigo pesa 065269999 kwa jina la mweka hazina wa klabu hiyo.
Alwan pia alisema kwa wadau wenye vitu vya kuchangia wanakaribishwa ikiwemo vifaa vya mazoezi, maji ya kunywa,madawa ya michezo na pesa kwa ajili ya posho za wachezaji ambapo wanaweza kufika kwenye mazoezi wanakofanyia uwanja wa Garden Kinondon.
Aidha, kwa upande wake Katibu Mkuu wa Villa, Mbarouk Kassanda alisema watahakikisha wanajituma kurejea ligi kuu ya Tanzania Bara msimu ujao licha ya kuwa kwenye kundi la kifo.
“Tumefikisha pointi saba na tupo nafasi ya nne, tunahakika kupanda hadi kileleni tutakapofanya vizuri kweye michezo yetu iliyobaki” alisema Kassanda.
Villa Squad |
Villa ipo kundi B, ikiwa na timu za Ndanda (Mtwara), African Lyon, Friends Rangers, Green Warriors , Polisi DSM, Tessema na Transit Camp zote za Dar es Salaam.
Ligi hiyo yenye kushirikisha jumla ya timu 24, iliyo kwenye makundi matatui huku kwa kila kundi ikitakiwa kutoa timu moja kupanda ligi kuu.
Makundi mengine ni kwa kundi A linaundwa na timu za Burkina Moro ya Morogoro, JKT Mlale (Ruvuma), Kimondo SC (Mbeya), Kurugenzi Mufindi (Iringa), Majimaji (Ruvuma), Mkamba Rangers (Morogoro), Polisi (Iringa) na Polisi (Morogoro).
Kwa upande wa kundi la mwisho ambalo ni kundi C, lina timu za JKT Kanembwa (Kigoma), Mwadui (Shinyanga), Pamba (Mwanza), Polisi (Dodoma), Polisi (Mara), Polisi (Tabora), Stand United (Shinyanga) na Toto Africans (Mwanza).
0 comments:
Speak up your mind
Tell us what you're thinking... !