Headlines News :
Home » » SIMBA WAUMBULIWA CECAFA

SIMBA WAUMBULIWA CECAFA

Written By Bashir Nkoromo on Thursday, November 28, 2013 | 1:53 AM

NAIROBI, Kenya
VIONGOZI wa klabu ya Simba wameumbuliwa na aliyekuwa wakala akimtafutia Juma Kaseja nafasi ya kucheza soka la kulipwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Wakala huyo, ambaye ni Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Sudani Kusini, Obanga Ismail, alisema viongozi hao ndio waliotia fitna ili Kaseja asisajiliwe nchini humo.

Obanga alisema ilikuwa tayari amekwishampatia nafasi Kaseja ya kuichezea klabu ya FC Lupopo na na Motema Pembe lakini baada ya taratibu zote kukamilika ndipo alipoanza kukutana na matatizo.

Alisema viongozi wa klabu ya Simba walipiga simu kwa viongozi wa FC Lupopo na Motema Pembe na kusema kuwa wasimsajili Kaseja kwa kuwa ni mtovu wa nidhamu.

Alisema pia viongozi hao waliwaambia viongozi wa klabu hizo kuwa Kaseja ni mpokea rusdhwa hivyo angeziharibu timu zao kwa vitendo hivyo.

"Kila kitu kilikuwa tayari n ilibaki Kaseja kwenda Congo kucheza kati ya timu hizo lakini viongozi wa Simba walimfanyia fitna," alisema.

Alisema kutokana na hali hiyo aliamua kuachana na Kaseja kwa kuhofia kupata matatizo licha ya kuzungumza na viongozi wa klabu hizo na kuwashawishi wamsajili mchezaji huyo.

Kaseja aliachwa na Simba mara baada ya mkataba wake kumalizika msimu uliopita kabla ya kusajiliwa na Yanga kwa kitita cha sh. milioni 40.
Share this article :

0 comments:

Speak up your mind

Tell us what you're thinking... !

Google+ Followers

Total Pageviews

Comments

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. theNkoromo Blog: SPORTS PAGE - All Rights Reserved
Template Design by Creating Website Published by Mas Template