Wachezaji wa timu ya Netiboli ya Temeke, wakiwa na mfadhili wa timu hiyo.Mbunge wa Temeke, Abbas Mtemvu kabla ya timu tiyo kuchuana jana na timu ya Katavi katika mechi ya fungua dimba ya michuano ya Netiboli Kombe la Taifa, kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
DAR ES SALAAM, TANZANIA
KATIKA kuiwezesha timu ya netibali ya Mkoa wa Temeke kuendelea kubaki na kombe la ubingwa ililolinyakua katika mashindano yaliyopita ya mprira huo Mbunge wa Temeke, Abbas Mtemvu, ameahidi kuisaidia timu hiyo kwa hali na mali.
Akizungumza wakati wa kuwakabidhi fedha za kijikimu kwa wachezaji wa timu hiyo, mwishoni mwa wiki katika ofisi yake, Mtemvu alisema yeye kama mdau wa michezo atahakikisha kombe hilo linabaki.
Katika hafla hiyo Mtemvu aliwakabidhi kiasi cha sh. 600,000 kama fedha za kujikumu kwa siku mbili kwanza na kuongeza kwamba atakuwa akifanya hadi pale mshindano hayo yatakapofikia tamati Januari 17, mwakani.
Kwa upande wake Nahodha wa timu hiyo,Malarena Muhagama, alisema, kama timu wamejipanga vilivyo kuhakikisha wanaendelea kuwa washindi katika mashindano hayo.
Muhagama alisema hilo linawezekana kabisa ukizingatia kwamba zaidi ya nusu ya wachezaji wao wanachezea timu ya taifa ya netiball.
Pia lisema katika kuhakikisha wanakuwa imara wakati wote wamekuwa wakifanya mazoezi kila siku na hivyo kuwaweka tayari wakati wote kukabiliana na timu shindani.
Kocha wa timu hiyo, Amina Musa, aliwataka mashabiki wa temeke kujijitokeza kwa wingi kuishangalia timu hiyo ambayo jana ilifungua mashindano na timu ya Katavi na kuibuka na ushindi wa mabao 48 kwa 15.
Mtemvu akisalimiana na wachezaji mbalimbali kabla ya michuano hiyo kuanza jana
Mchezaji wa timu ya Temeke Sekela Mwakanyuki (kulia) akitafuta njia ya kumpenya mchezaji wa Katavi Rose Ezrael, katika mechi hiyo jana.
Mchezaji wa Katavi akijaribu kuumiliki mpira
Mchezaji wa TMK akimdhibiti mchewzaji wa Katavi asaipate bao langoni
Hekaheka katikati ya uwanja wakati wa mechi hiyo
Mchezaji wa Temeke akipachika bao golini mwa Katavi. Katika mechi hiyo Temeke iliibuka mshindi kwa mabao 58-27
Home »
» MICHUANO YA NETIBOLI TAIFA YAANZA, MTEMVU APANIA TEMEKE IENDELEE KULISHILIKIA KOMBE
0 comments:
Speak up your mind
Tell us what you're thinking... !