Headlines News :
Home » » MWILI WA ALIYEKUWA KOCHA WA MAKIPA SIMBA, JAMES KISAKA WAAGWA LEO MUHIMBILI, KUZIKWA KESHO KIJIJINI KWAO LUSANGA, MUHEZA MKOANI TANGA

MWILI WA ALIYEKUWA KOCHA WA MAKIPA SIMBA, JAMES KISAKA WAAGWA LEO MUHIMBILI, KUZIKWA KESHO KIJIJINI KWAO LUSANGA, MUHEZA MKOANI TANGA

Written By Bashir Nkoromo on Thursday, December 26, 2013 | 9:56 AM

 Benny Kisaka ambaye ni mdogo wa marehemu James Kisaka ambaye alikuwa Kocha wa Makipa wa timu ya Simba, akisoma wasifu wa marehemu, wakati wa shughuli ya kuaga mwili, iliyofanyika leo jioni, katika Kanisa la KKKT, Muhimbili jijini Dar es Salaam, Kwa mujibu wa Benny, Msafara utaondoka kesho alfajiri kwenda katika Kijiji cha Lusanga, Muheza mkoani Tanga ambako marehemu Kisaka atazikwa mida ya saa saba mchana.
 Mwenyekiti wa Chama Cha Waandishi wa habari za michezo, Juma Pinto (kulia) akiwa pamoja na waombolezaji wengine wakati wa kuaga mwili wa marehemu James Kisaka
 Waombolezaji, wake kwa waume, wakisubiri kuaga mwili wa marehemu James Kisaka
 Waombolezaji wakifuatilia misa ya kuaga mwili wa marehemu James Kisaka
 Benny Kisaka akiwaeleza waombolezaji taratibu zinazofuata baada ya kuagwa mwili wa marehemu
 Waombolezaji wakitia heshima za mwisho
 Wapenzi wa soka na wale wa sanaa wakitoa heshima zao za mwisho
 Katibu Mkuu wa Yanga, Mwalusako akitoa heshima za mwisho
 Kocha msaidizi wa zamani wa Simba, Julio, akitoa heshima za mwisho
 Julio akinmkumbatia kwa majozi mdogo wa marehemu, Benny Kisaka baada ya kutoa heshima za mwisho
 Mtoto wa mwisho wa marehemu James Kisaka, Christopher na muombolezaji aliyemsindikiza wakilia baada ya kutoa heshima za mwisho
 Boniface James, ambaye ni mtoto wa pili wa Marehemu James Kisaka, akiuaga mwili wa marehemu baba yake.
 Boniface akilia huku akisaidiwa na rafiki zake baada ya kuaga mwili wa marehemu baba yake
 Teddy ambaye ni mjane wa marehemu James Kisaka akitoa heshima za mwisho
 Boniface akiwa ameshika msalaba wa marehemu Baba yake wakati jeneza lenye mwili lilipokuwa limetolewa nje tayari kupakiwa katika basi kwa ajili ya afari ya kesho kwenda Tanga
 Waombolezaji wakipakia jeneza kwenye basi ya Klabu ya Simba kutoka Muhimbili
Baadhi ya wadau wa Soka akiwemo Jamal Rwambo, wakiwa wenye huzuni wakati wa kuaga mwili wa marehemu James Kisaka.
Share this article :

0 comments:

Speak up your mind

Tell us what you're thinking... !

Google+ Followers

Total Pageviews

Comments

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. theNkoromo Blog: SPORTS PAGE - All Rights Reserved
Template Design by Creating Website Published by Mas Template