Headlines News :
Home » » HAFLA YA CHAKULA CHA JIONI KILICHOANDALIWA NA KINANA KWA WAANDISHI WA HABARI NA WASANII BAADA YA SHEREHE ZA MIAKA 37 YA CCM JIJINI MBEYA

HAFLA YA CHAKULA CHA JIONI KILICHOANDALIWA NA KINANA KWA WAANDISHI WA HABARI NA WASANII BAADA YA SHEREHE ZA MIAKA 37 YA CCM JIJINI MBEYA

Written By Bashir Nkoromo on Monday, February 3, 2014 | 12:05 AM

 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza na waalikwa kwenye hafla ya chakula cha jioni kilichoandaliwa na Katibu Mkuu wa CCM,Abdulrahman Kinana kwa ajili ya waandishi wa habari na wasanii baada ya sherehe za maadhimisho ya miaka 37 ya CCM, zilizofanyika Februari 2, mwaka huu jijini Mbeya. Hafla hiyo ya chakula cha jioni ilifanyika  kwenye ukumbi wa Halmashauri ya Mji wa Mbeya.
 MKurugenzi wa Tanzania One Theatre (TOT) Kapteni John Komba akizungumza  wakati wa hafla hiyo ya chakula cha jioni.
 Wasanii wakimpongeza Kapteni John Komba kwa wosia mzuri aliotoa juu yao .
 Msanii Maarufu nchini Hafsa Kizinja akitumbuiza siku ya usiku wa Wasanii na Waandishi wa Habari,Februari 2 mjini Mbeya ,siku ambayo CCM ilisheherekea miaka 37 ya kuzaliwa kwake na kitaifa sherehe hizo zilifanyika mjini hapo.
 Waandishi wa habari kutoka vyombo mbali mbali waliokuwa kwenye sherehe za miaka 37 ya CCM jijini Mbeya, wakimshangilia Mwenyekiti wao Richard Mwaikenda baada ya kuzungumza kwa niaba yao kwenye chakula hicho cha jioni.
 Wasanii wa tasnia ya Filamu wakiwa wamepozi kwenye hafla hiyo ya chakula cha jioni
 Msanii wa Siku Nyingi nchini Dokii akisalimiana na  Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara) Mwigulu Lameck Nchemba ambaye pia ni  Naibu Waziri Wizara ya Fedha (Sera) wakati wa hafla hiyo
 Baadhi ya waandishi kutoka Jjiji la Mbeya wakipata vinywaji na maongezi kidogo wakati wa hafla hiyo.
 Waandishi wa Umoja wa Waandishi wa Habari mkoani Mbeya wakizungumza na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana wakati wa hafla hiyo ya chakula cha jioni.
 Wasanii wakongwe wa tasnia ya filamu Tanzania nao walikuwepo kutoka kushoto ni Baba Haji, JB na Rich.
 Kila mtu maarufu alikuwepo kwenye tasnia ya sanaa za maigizo na filamu.
 Malkia wa Taarab nchini Hadija Kopa akitoa vionjo vya wimbo wake mpya wa 'Mimi Maarufu'.
Katibu wa NEC Itikadi na Unenezi wa CCM Nape Nnauye akicharaza gita na kuimba na kundi la TOT wakati wa  hafla hiyo.
Share this article :

0 comments:

Speak up your mind

Tell us what you're thinking... !

Google+ Followers

Total Pageviews

Comments

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. theNkoromo Blog: SPORTS PAGE - All Rights Reserved
Template Design by Creating Website Published by Mas Template