*Wamo magwiji: Ally Remutulla, Mustapha Hassanal, Khadija Mwanamboka, Martin Kadinda
*Chipukizi wamo Faustin Simon, Water Edward,Willex Willibard, Jackson, Alabama King
Na Andrew Chale
WABUNIFU mbali mbali watakaopamba miaka 10 ya onyesho la
mavazi lijulikanalo kama ‘Lady in red Super brand, 10th Anniversary’
linalotarajiwa kufanyika Februari 14, tayari majina yao yamewekwa hadharani. Onyesho la mwaka huu
linatarajia kufanyika kwenye hoteli ya Serena, jijini Dar es salaam, Februari 14, huku asilimia ya
mapato ya fedha hizo zinatarajia kusaidia wathirika wa dawa za kulevya wa kituo
cha Kikale Kilichopo Mkoani Pwani.
Akizungumza na wandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Fabak
Fashions inayoandaa onyesho hilo, Asia Idarous
Khamsin (pichani), alisema kila mwaka onyesho hilo
huja kitofauti ikiwemo kuongeza vionjo mbalimbali katika kufikia mafanikio
kwenye tasnia ya ubunifu na mitindo ya mavazi
hapa nchini.
“Safari hii, steji ya Lady in red’, inatimiza miaka 10, huku
ikijivunia kuibua vipaji vya wabunifu wengi hapa nchini, na wengine kwa sasa
wanamajina makubwa kwenye yasnia hiyo, hivyo tutaendelea kutoa nafasi kwa
wabunifu chipukizi mara kwa mara ilikufikia malengo yao” alisema Asia Idarous.
Asia Idarous aliwataja wabunifu magwiji watakaopamba steji
hiyo kuwa ni pamoja na Khadija Mwanamboka, Mustapher Hasanal , Ally Remtulla,
Lucky Creation, Martin Kadinda, Ghymkana Hilali, Paka wear, Gabriel Molel, Fransiska
Frankoo, Shirima, Salim Ally, Ameed
Abdul, Mgese Makory, Kiki Collection, Rose fashion, Diana Magesa, Rio Paul na
wengine.
Kwa upande wa wabunifu chipukizi watakaopamba ni pamoja na
Faustin Simon, Water Edward, Brian Hango, Benedict Mnzava,Crissiwelly Uissoson,Willex
Willibard, Jackson, Gumbala, Jabir
Jumanne, Alabama King, Agusta Masaki, Nelson Tomas, Bebi Juliet Mtandu, Ummi
fashion/Ummi Investiment Comapany, Asmahan Eva, Hassan Nasor, Juniper Mafuru,
Ante Ngongi, Adam Hassan, Jaquline, Kijangwa na Waiz Shelukindo.
Aidha, Asia Idarous aliongeza kuwa, kwenye onyesho hilo, pia kutakuwa na
burudani mbalimbali ikiwemo kutoka bendi ya Babloom Trio na Mwanamuziki mahiri
wa nyimbo na ngoma za asili, Wanne Star. Katika onyesho hilo ambalo litafanyika siku hiyo ya Februari
14, ambayo pia itakuwa ni siku ya Wapendanao ‘Valentine’s Day’ , kiingilio
kitakuwa sh 30,000 kwa viti vya kawaida huku viti maalum ikiwa sh 50,000.
Tayari tiketi za onyesho hilo zimeanza kuuzwa ikiwemo vituo vya duka
la Fabak fashion, lililopo mikocheni mkabala na kituo cha Mwalimu Nyerere huku
kwenye hoteli ya Serena, zikipatikana mapokezi.
Kwa upande wa wadhamini wakuu wa shindano hilo ni pamoja na kinywaji cha Zanzi pamoja
na kampuni ya nywele ya Darling. Wengine ni CXC, Times fm, Clouds media,
Vijimambo blog, michuzi media group, channel ten, Elite Computer, Eventlites,
One touch-solution, Raysa Style, Paka Wear, Dj Bula, Magic fm, DTV, Jambo Leo,
I View media, Vayle Spring, Voice of American na wengine wengi.
0 comments:
Speak up your mind
Tell us what you're thinking... !