Headlines News :
Home » » BEKI WA ZAMANI WA ARSENAL, EMMANUEL EBOUE ATUA SUNDERLAND ILIYOPO LIGI KUU YA ENGLAND (EPL)

BEKI WA ZAMANI WA ARSENAL, EMMANUEL EBOUE ATUA SUNDERLAND ILIYOPO LIGI KUU YA ENGLAND (EPL)

Written By Bashir Nkoromo on Friday, March 11, 2016 | 1:53 AM

Emmanuel-Eboue
Emmanuel Eboue akipozi na jezi ya  Sunderland.
BEKI wa zamani wa Klabu ya Arsenal, Emmanuel Eboue, amejiunga na timu ya Sunderland inayoshiriki Ligi Kuu ya England (EPL). Eboue, mwenye umri wa miaka 32, alikuwa mchezaji huru baada ya kuondoka Galatasaray ya Uturuki mwanzoni mwa msimu huu.
eboue
Akiwa na Galatasaray kuanzia 2011, Eboue alifanikiwa kutwaa ubingwa wa ligi hiyo mara tatu pamoja na makombe mengine matano.
Eboue aliichezea Arsenal kwa misimu minane baada ya kutua hapo mwaka 2004 kutoka klabu ya Ubelgiji ya Beveren na kisha kuhamia Galatasaray mwaka 2011.

Sunderland imempa mchezaji huyo mkataba wa muda mfupi ambao utamalizika mwishoni mwa msimu.
Share this article :

0 comments:

Speak up your mind

Tell us what you're thinking... !

Google+ Followers

Total Pageviews

Comments

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. theNkoromo Blog: SPORTS PAGE - All Rights Reserved
Template Design by Creating Website Published by Mas Template