0713682040,0767682041
Makala
hii inalenga kutoa mafunzo muhimu ya dhana juu ya utafiti wa hivi karibuni juu
ya Sayansi ya Soka na matumizi ya
mazoezi madogomadogo (Multiple Small Sided Games) katika kubaini, kuendeleza
vipaji vya vijana wanaochipukia kutika soka kwa kutimia elimu mwendo kwa
binadamu (Human Kinetics) ili kupata mafanikio katika soka la dunia ya leo.
Ni
ukweli usiopingika kuwa changamoto ya ushambuliaji dhidi ya Ulinzi bado
inaendelea (Jay Miller: 2014) hususani nchini Tanzania, katika makala hii
tutabaini stadi, ufundi na mbinu muhimu za Kisayansi za kuvunja mipango iliyoratibiwa
ya ulinzi katika soka. Ili timu yeyote
iweze kufanya mashambulizi yenye mafanikio inapaswa kutengeneza fursa kwenye
theluthi ya ushambuliaji (John Hackeworth: 2014) kam umoja na uwili(One
Twos),mchezo wa kupishana(Overlap),Pasi Jozi(Double Pass),Ufungaji wa magoli 4
kwa kukimbia(Four Goal shooting on the Run),muungano wa wachezaji watatu kufunga(Three Man Combinations to Goal),Mchezo wa magoli 3 na faida ya
ongezekeo la namba(Three Goal Numerical Advantage Gama),Upishanaji wa
kufunga(Ovelapping to score) Mpito(3v2 to 4v3 Transition) na Ruwaza ya
Goli(Pattern Play to Goal).
Ni muhimu kutumia uchezaji wa Kimuungano
(Combination Play) ambao unaweza kusababisha umaliziaji na ufungaji wa kisayansi
(Finishing and Shooting) kwa kutumia mbinu zifutazo za uchezaji wa kimuungano
kama Ukaguzi kabla ya ndege kupaa(Check in),Uchukuzi wa kisigino(Heel
Takeover), uchukuzi mshazali(Staight Takeover), kupitiliza(Overlap) na Zunguka
uso kimbia(Round the face Run).
Ili
timu yeyote iweze kuwa na falsafa na mkakati wa mashambulizi wenye mafanikio
sharti washambulie kupitia pembezoni (Dean Wurzberger: 2014) kwa kutumia
mazoezi kama;kikosi cha kupiga mipira ya mkato na umaliziaji (Squad scrossing
and Finishing),Rajua ya upitilizaji wa wachezaji watatu (Three Player Overlap Pattern),Umalizaiaji
wa mielekeo mitatu(Two direction finishing),Mipira ya Mkato na umaliziiaji
katika theluthi ya mwisho, mchezo wa wiga 8v8(8v8 Winges Game), Mbawa huru za
kupigia mipira ya mkato(Free Wing Crossing Boxes) ,Uchezaji wenye manufaa wa
pembezoni (Functioal Flank Play),Mashambulizi ya pembezoni ya wachezaji 9 dhidi
ya 9 (9v9 Flank Attack) kama jinsi ambavyo timu za Simba na Yanga
zinavyotegemewa kufanya kwa kawaida, vinginevyo kwa kuzingatia falsafa ya
umiliki wa mpira falsafa na mkakati wa ushambuliaji unaweza kupitia katika
theluthi ya kati (Ken Lolla: 2014) kwa kutumia mazoezi kamaUmiliki kuelekea
malengo(Possession to Targets),Mtafute mshambuliaje uende naye(Find The
Forrward nd Go),Mchezo wa magoli mengi(Multiple Goal Game),Mchezo wa Magoli
sita(Six Goal Game),Funga ndani ya dakika % Ushinde(Score in Five To Survive),
kama ambavyo timu za Azam na Simba ambavyo hutarajiwa kucheza. Wakati mwingine mashambulizi huweza kufanyika
kutoka theluthi ya ulinzi (Mike Noonan: 2014) kwa kutumia mazoezi kama;pass
mruko na uzungushaji wa mpira (Skip pass and ball Rotation),Hatua za mwanzo wa
ujenzi wa ushambuliaji kutoka nyuma (GK+5v3 to 3v5+GK) ,mwelekeo wa
pembezonikushambulia(Advancing the Wingbacks to Attack),Uvunjaji wa msongo
wachezaji 9 dhidi ya 6(9v6 Breaking Pressure) na Mashambulizi ya wachezaji Kumi(Ten Attacks) kama ambavyo timu za Simba
na Yanga zinavyotarajiwa kucheza.
Walakini
timu vyingi hazina Stadi, Mbinu na Ufundi wa kutosha kuelewa na kutumia michezo
midogomidogo ya kurudiwa, kwata na mazoezi (Multiple Small Sided Games and Drills)
ili kuanzisha kuratibu na kutenda mashambulizi ya kisayansi nchini. Hata mazoezi ya kupasha yanayofanyika kabla
ya mechi kuanza kueleza hualisia huu kwa kuzingatia mawanda ya udukuzi katika
soka (Soccer Intelligence) (Dick Bate & Ian Jeffreys: 2015).
Mfululizo
wa makala hii unalenga kuonyesha uhitaji
mkubwa uliopo na pengo lililopo nchini katika kufundisha Sayansi ya Soka na hususani
Elimu Mwendo Binadamu (EMB) yaani (Human Kinetics). Mwandishi wa mada hii na wadau wengine wa
sayansi ya soka wanalenga kuanzisha Chuo cha Sayansi ya soka hapa nchini.
Hivi sasa wapo katika hatua za mwisho za
kuandaa mitaala na kupitia mchakato wa Usajili wa Chuo hicho ili kutatua tatizo
hili ambalo linachagia kudidimiza soka la Tanzania.
Makala hii pia inalenga kufanya uoni
(Observation) wa kisayansi katika viwango vya matumizi ya michezo midogomidogo
ya kurudiarudia na kwata (multiple small sided games and drills) za sayansi ya
soka la ushambuliaji na falsafa zake katika timu 3 kubwa za Tanzania ambazo ni
Simba, Yanga na Azam wakati wa ligi kuu mwaka 2016/2017.
Lengo la makala hizi ni kuzijengea uwezo timu
hizi kuona umuhimu wa walimu, wachezaji, wachambuzi, wawekezaji katika soka,
wadhamini wa soka, watangazaji wasoka, wabashiri wa soka, watazamaji wa soka na
wapenzi wa soka kuelewa soka la kisayansi na kuliendeleza soka la Tanzania
kisayansi. Aidha timu nyingine za ligi
kuu, na madaraja mengine ya kwanza, pili, tatu na nne kitaifa, kimikoa,
kiwilaya yataweza pia kulielewa soka la kisayansi kwa lugha rahisi ya Kiswahili.
Makala hii inalenga pia kujenga uwezo wa vijana
wanaochipukia wenye vipaji vya soka ili waweze kuelewa na kutumia stadi, mbinu
na ufundi wa kisayansi ili kuendeleza vipaji vyao hata kama wanaelimu ya
kiwango kidogo kwa kutumia stadi, mbinu na ufundi wa elimu mwendo binadamu
(Humana Kinetics). Ayumkini tutaweza
kuendeleza soka la Tanzania.
Nilipomuhoji
mmoja wa wanagunzi wa Chuo cha soka cha Elimu mwendo wa binadamu (Human Kinetics Academy) Stanford
Andambike ambaye ni mshambuliaji (Striker) juu ya mehci ya Simba na Azam
alikuwa na haya ya kusema.
Japokuwa
mchezaji Shiza Kichuya aliyefunga goli, yeye alinukuliwa kusema na vyombo vya
habari kuwa “Kocha aliniambia nipige shitu nje ya kumi na nane”.
Mwanafunzi
Stanford Andambike kutoka Human Kinetics Academy alisema “Simba wametumia
falsafa ya wachezaji wote kushambulia wote kulinda na soka la mguso mmoja kwa
mfumo wa 4:4:2. Yawezekana alisema hivyo kwa vile hiyo ndiyo falsafa
inayosisitizwa kule chuo cha Human Kinetics Academy.
Tuseme hapa bayana kuwa mfumo huu unafaida ya
timu kujibana (Compact) ila unapaswa kuwa yabisi (solid) katikati na
unawawezesha viungo kuwasaidia walinzi na washambuliaji kwa urahisi. Faida yake kubwa ni kwamba ni mfumo rahisi
maranyingi kubadili katika 4-4-2 kwenda kwenye mfumo wa ushambuliaji zaidi wa
4-2-4 au hat 4-3-3 bila kuwa na uharibifu kwa wachezaji au mahitaji ya
kubadilisha wachezaji.
Ni mfumo unaofaa
kwa kuwaruhusu wachezaji wa viungo kuwasaidia washambuliaji na walinzi (Patrick
Morgan: 2006). Tuseme bila kigugumizi kuwa mfumo kama 4-3-3 ambayo
hubadilika na kuwa 4-5-1 wakati wa ulinzi na 4-4-2 ambao hubadilika na kuwa
4-4-1-1 wakati wa ulinzi mshambuliaji akichukua nafasi ya kiungoni wakati mwingine
timu hucheza zaidi na kiungo kuliko
5-1-4 kwenye nusu yao ya uwanja wanapojilinda na katika jaribio la kuzuia
bunduki kubwa, mifumo hii kwa sasa siyo muhimu sana kwa malengo iliyobuniwa
kuyatekeleza.
Mameneja wengi duniani wa
Timu huamini kuwa dhana ya mifumo washambuliaji wanavyohusika na kupaswa
kutenda ni mifumo inayokufa taratibu.
Nafasi ya mifumo hii sasa inachukuliwa na washambuliaji 6 ambao wanaweza
kubadilishana nafasi wakati wakusaidiwa na mabeki wa kushoto(full backs0 katika
soka la kileo kuna mifumo mipya inayotokana na mapinduzi ya soka la
ushambuliaji (Revolution in attacking football). Beki wa kushoto (full baks) leo ndio
wachezaji muhimu katika kikosi cha mashambulizi na wanaotizamwa zaidi katika
timu (The Secret Footballer’s Guide to the modern Game, page 158). Kwa mantiki hiyo mimi naziangalia timu zetu
kwa kuwaangalia Malika Ndeule (Simba), Haji Mwinyi (Young Africans sc), Bruce
Kangwa (Azam Fc) na kwa soka la Tanzania lijalo kwa kazi nzuri ya Serengetii
Boys namwangalia Nickson Clement Kibabage na uwezo wao katika stadi, mbinu na
ufundi wa Kisayansi.
Kuna
mifumo mingi ya kileo kama; 4-2-3-1 katika mfumo huu (fullbacks) wote wawili
wanaweza kwenda mbele muda mmoja na timu inaweza kushambulia mara moja kwa
kutumia wachezaji hadi 8. Sharti
wachezaji na viungo waratibiwe pande zote.
Hapo kuwa mfumo huu unatishio la mashambulizi ya kushitukiza (counter
attack) pembeni chini. Aidha (fullbacks)
sharti wawe imara kwani pia hutakiwa kucheza kama winga. Mfumo huu unatishio la kuathiriwa na timu
yenye washambulizi imara wa kati.
Katika
mfumo wa 3-5-2 wachezaji winga (winbacks) ndio muhimu katika mafanikio ya mfumo
huu. Kifo cha mfumo wa 4-4-2
kimesababisha kuzaliwa kwa zama mpya za mikakati na mifumo katika soka.
Kuna
baadhi ya wachambuzi wanahusisha zama hizi na kifo cha winga. Nafasi zao zinachukuliwa na fullbacks na
viungo washambuliaji wenye vipaji. Hawa
hupeleka mipira pembeni. Kuondoka kwa
winga kunafanya fullbacks waweze kushiriki katika ushambuliaji wanapojisikia,
leo mashambulizi mengi yanaanzishwa na fullbacks na ndio wachezaji timamu zaidi
katika timu.
Dunia imeshuhudia timu ya
Manchester United wakimsainisha mkataba kijana wa miaka 18 kutoka Southapton
kwa paundi milioni 30 akivunja rekodi ya vijana wanaochipukia.
Mwanafunzi
Stanford Andambike aliendelea kusema kuwa pia Simba walikuwa wanashambulia
kupitia winga hususani Ibrahim Ajib. Na
pia Simba wametengeneza fursa za kufunga kupitia kucheza umoja uwili (0ne-Twos)
Shiza Kichuya na Ibrahim Ajib na Laudit Marugo na Ibrahim Ajib.
Kwa maelezo yake pia wamecheza uchezaji wa
kimuungano wa umaliziaji na upigaji shuti (Finishing and Shooting) uchukuzi
mnyofu (Straight Takeover) kati ya Ibrahim Ajib na Shabalala .
Joseph
Omog ambaye ni Coach wa Simba, Jackson Mayanja ambaye ni Kocha msaidizi,
Technical Advisor Hassan Selemani na Mussa Hassani Mgosi ambaye ni meneja wa timu wanafahamu kuwa walipanga kufanya
nini zaidi. Wanafahamu falsafa, mfumo na
mikakati waliyoipanga na kutekeleza hata itakayotumika tarehe 1 Oktoba 2016
dhidi yon a watani wao wa jadi Yanga.
Aidha
kwa upande wa Azam kocha Zeben Harnandes na msaidizi wake Yeray Romero na
mshauri wao wa ufundi Pablo Borge sambamba na meneja wao Simon Alando
wanajua falsafa waliyolenga kutumia na
mkakati waliojiwekea na mfumo husika.
Aidha
kama tulivyokwisha sema hapo awali mfumo waliotumia Azam wa 3-5-2 unategemea
sana wingbacks ili uwe na mafanikio. Beki
mfagizi (Sweeper) kwa maana hiyo Himid Mao pekee ndiye alitarajiwa kuwa bila
msongo na mpira. Hatuna uhakika kama
Azam hucheza na Mfagizi (Sweeper).
Japokuwa mfumo huu hubadilika na kuwa 4-1-4-1 na hii hutokea wakati timu
hucheza na mshambuliaji mmoja na namba 10 ambaye alipaswa kuwa Shaban
Chilunda. Wengi hutizama mfumo huu kama
njia ya kuhifadhi nguvu kwenye mechi kwani wachezaji wachezao kwenye kiwango
cha juu cha uchezaji wao ni winga na nyma (wingbacks) ambao mara nyingi
hushambulia. Kama tulivyokwisha sema
fullbacks siku hizi ndio wingbacks ambao hupasha kuwa timamu kuliko wachezaji
wote uwanjani. Ikimaanisha kuwa beki
wako (center half) hawapendi kwenda pembeni (wide curves) kulind kwani hufanya
………….. …
Kuna mengi unapaswa kutumia waachezaji ulionao kutumia mfuno unao
iwezesha timu kucheza vizuri. Ukweli ni
kwamba kwa kutumia mfumo wa 3-5-2 ni rahisi kufanya mshambulizi ya kushtukiza
kama timu itakaa nyuma na kusahau hatari ya wingback. Timu ikiamua kucheza kasi ya mchezaji huwa
rasilimali kubwa ya mfumo kama Arjen Robben wa spain
0 comments:
Speak up your mind
Tell us what you're thinking... !