Headlines News :
Home » » BONDIA MTANZANIA ULINGONI OLIMPIKI KESHO JUMAPILI

BONDIA MTANZANIA ULINGONI OLIMPIKI KESHO JUMAPILI

Written By Bashir Nkoromo on Saturday, July 28, 2012 | 4:50 AM

Bondia Selemani Kidunda katikati akiwa kwenye picha ya pamoja na wawakilishi wengine wa Tanzania kwenye Olimpiki 2012. Kesho Kidunda anapanda ulingoni kumvaa raia wa Moldova.
Baadhi ya wawakilishi wa Tanzania kwenye mashindano ya Olimpiki 2012 jijini London, wakishikilia bendera ya taifa wakati wa sherehe za ufunguzi juzi Ijumaa.
Baadhi ya wawakilishi wa Tanzania kwenye mashindano ya Olimpiki 2012 jijini London, wakipozi kwa picha wakati wa sherehe za ufunguzi juzi Ijumaa.

LONDON, England
Bondia wa ngumi za ridhaa, Mtanzania Seleman Kidunda, kesho Jumapili anapanda ulingoni kuanza kupeperusha bendera ya taifa kwenye mashindano ya Olimpiki yaliyozinduliwa juzi Ijumaa jijini London.

Kidunda, 28, ambaye ni bondia pekee kupata tiketi ya kucheza mashindano hayo katika mchezo wa ngumi za ridhaa nchini, anapanda ulingoni kuumana na Belous Vasilii, 23 raia wa Moldova.

Mshindi kati ya Kidunda na Vasilii, atakuwa na kazi ya ziada wakati atakapotakiwa kupanda tena ulingoni hapo Agosti 3, kuzipiga na Shelest Yuk wa Ukraine, ambaye yeye ameingia hatua ya pili kutokana na ubora wake.

Pambano kati ya Kidunda na Vasilii ambalo ni la uzzito wa Kilo 69, upande wa wanaume, litatanguliwa na mapambano mengine 12 ya ngumi leo.
Share this article :

0 comments:

Speak up your mind

Tell us what you're thinking... !

Google+ Followers

Total Pageviews

Comments

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. theNkoromo Blog: SPORTS PAGE - All Rights Reserved
Template Design by Creating Website Published by Mas Template