Headlines News :
Home » » NGASSA RASMI SIMBA, AKABIDHIWA JEZI NO 16 LEO

NGASSA RASMI SIMBA, AKABIDHIWA JEZI NO 16 LEO

Written By Bashir Nkoromo on Friday, August 3, 2012 | 8:36 AM

DAR ES SALAAM, TANZANIA
MCHEZAJI mpya wa Simba, Mrisho Ngassa, leo amekabidhiwa jezi namba 16 atakayokuwa akiitumia kwenye klabu yake msimu huu.

Ofisa habari wa timu hiyo, Ezekiel Kamwaga amesema, Ngassa alikabidhiwa jezi yake hiyo katika makao makuu ya Simba Mtaa wa Msimbazi jijini Dar es Salaam na Makamu Mwenyekiti wa Simba, Geofrey Nyange Kaburu.

Kaburu alisema Simba inamkaribisha Ngassa kwa moyo mmoja na kwamba wapenzi wote wa Wekundu wa Msimbazi wana imani kubwa naye kwani uwezo wake mkubwa wa soka unafahamika ndani na nje ya nchi.

"Tunashukuru kwamba tumekidhi vigezo vyote vilivyohitajika kwa ajili ya usajili wa mchezaji huyu. Tumeingia naye mkataba wa mwaka mmoja baada ya kumaliza muda wa mkopo wake kutoka Azam na ni imani yetu kwamba ujio wa Ngasa utaimarisha zaidi timu kwani yeye ni miongoni mwa wachezaji ambao Kocha Mkuu wa Simba, Milovan Cirkovic, anawapenda," alisema.

Akizungumza katika tukio hilo, Ngassa alisema amefurahi kusajiliwa na Simba kwani ni sawa na historia kujirudia, akikumbusha kwamba baba yake mzazi, Khlfan Ngassa, aliwahi kuwa mchezaji wa klabu katika miaka ya 1990.

Kabla ya mkutano huo na waandishi wa habari, Ngassa alifanya mazoezi na wachezaji wenzake wa Simba katika ufukwe wa Coco, jijini Dar es Salaam ambako Simba inaendelea na mazoezi yake chini ya makocha Amatre Richard na James Kisaka.
Share this article :

0 comments:

Speak up your mind

Tell us what you're thinking... !

Total Pageviews

Comments

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. theNkoromo SPORTS - All Rights Reserved
Template Design by Creating Website Published by Mas Template