Headlines News :
Home » » BANDARI YAJIWEKA PAZURI LIGI YA GRAND MALT ZANZIBAR

BANDARI YAJIWEKA PAZURI LIGI YA GRAND MALT ZANZIBAR

Written By Bashir Nkoromo on Sunday, September 30, 2012 | 9:10 AM


Na Mwandishi Wetu, Zanzibar
LIGI Kuu ya Soka ya Grand Malt ya Visiwani hapa iliendelea juzi kwa timu ya Bandari kuibuka na ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Mundu katika mchezo uliofanyika kwenye Uwanja wa Amaan.

Katika mchezo huo uliokuwa na ushindani wa pande zote mbili karibu muda wote wa mechi, ilikuwa ni dakika ya 42 ambapo Bandari walifanikiwa kupata goli pekee kupitia kwa mshambuliaji wake, Hissam Hamis.

Hata hivyo washambuliaji wa Mundu pia hawakuwa makini kwenye mchezo huo kutokana na kupoteza nafasi mbalimbali walizotengeneza na kuishia kupiga mashuti pembeni ya kusababisha wapoteze pointi tatu muhimu kwenye ligi hiyo.

Katika mchezo mwingine uliofanyika Pemba kwenye Uwanja wa Gombani, mabingwa wa zamani wa ligi hiyo, Jamhuri waligawana pointi na Mtende ambayo imepanda daraja msimu huu baada ya dakika 90 kumalizika wakiwa na sare ya goli 1-1.

Ligi hiyo ilitarajiwa kuendelea tena jana jioni kwa kuzikutanisha timu za Malindi dhidi ya Chuoni kwenye Uwanja wa Amaan wakati huko Pemba Chipukizi wataikaribisha Mafunzo kwenye Uwanja wa Gombani jioni na leo Dume itavaana na Mtende jioni huku usiku Falconwatachuana na Mafunzo.

Kampuni ya Bia Tanzania kupitia kinywaji chake kisicho na kilevi ndio wadhamini wakuu wa ligi hiyo inayoshirikisha timu 12 kutoka Unguja na Pemba.

Mshindi wa kwanza wa ligi hiyo ataiwakilisha Zanzibar katika mashindano ya Klabu Bingwa Afrika mwakani pamoja na michuano ya Kombe la Kagame huku mshindi wa pili atapeperusha bendera ya Zanzibar kwenye mashindano ya Kombe la Shirikisho
Share this article :

0 comments:

Speak up your mind

Tell us what you're thinking... !

Google+ Followers

Total Pageviews

Comments

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. theNkoromo Blog: SPORTS PAGE - All Rights Reserved
Template Design by Creating Website Published by Mas Template