Headlines News :
Home » » TASUBA KITUO BORA CHA SANAA NA UTAMADUNI AFRIKA MASHARIKI

TASUBA KITUO BORA CHA SANAA NA UTAMADUNI AFRIKA MASHARIKI

Written By Bashir Nkoromo on Sunday, September 30, 2012 | 8:47 AM


NA MAGRETH   KINABO – MAELEZO
TAASISI ya Sanaa na Utamaduni, (TaSuBa) iteuliwa kuwa Kituo bora kilichotuka  cha Sanaa na Utamaduni cha  Afrika Mashariki.

Kauli hiyo ilitolewa jana na Mtendaji Mkuu wa taasisi hiyo, Juma Bakari  katika sherehe za mahafali ya 23 ya wahitimu mbalimbali wa sanaa na utamaduni yaliyofanyika katika ukumbi wa  TaSUBa, Bagamoyo mkoani Pwani.

“Tulianza tukiwa mchicha mwaka 1981 sasa tumekuwa mbuyu mwaka 2012, shikamaneni,|’’ alisema.

Aliongeza kuwa wamejipanga kukabiliana vizuri na changamoto zilizopo ilikukidhi haja ya ubora wa taasisi hiyo katika nchi  za Afrika Mashariki, ambazo ni miundombinu, ukuzaji wa mitaala, wakufunzi wa kutosha.

Akizungumzia kuhusu suala hilo, mgeni rasmi katika mahafali  hayo ,ambaye ni Mweyekiti  wa Bodi ya    Ushauri ya taasisi hiyo ambaye ni Mhadhili katika Chuo Kikuu cha Dares Salaam(UDSM), Profesa  Elias Jengo alisema uteuzi huo ni heshima kubwa kwa nchi ya Tanzania.

Profesa Jengo alisema mchakato huo ualinza tangu mwaka 2002 na hatimaye  hivi karibuni mwaka mwaka huu taasisi hiyo imepata ubora huo. Aliongeza kuwa  hiyo ni   heshima  haijawahi kutokea katika kipindi cha miaka 36 ya UDSM katika kufundisha fani hizo.

Akizungumzia kuhusu suala hilo, Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya  Utamaduni kutoka Wizara ya Habari, Vijana ,Utamaduni na Vijana, Profesa Hermas Mwansoko alisema ubora huo umefanya wahitimu wa taasisi hizo kuweza kufanya kazi mahali popote katika nchi hizo.

Naye Mkuu wa Idara ya  Taaluma wa taasisi hiyo, Michael Kadinde alisema uteuzi huo umefuatia baada jopo la wajumbe wa watu watano kutoka nchi za Afrika Mashariki, wakiongozwa na Mwenyekiti wao kupitia vyuo vyote vinavyotoa taaluma hizo kwa kuangalia  masuala ya utawala, mafunzo, miundombinu na malipo ya wafanyakazi.

Aidha alisema Wizara husika imekuwa ikipigania  mfumo wa utendaji kazi wa sekta ya Utamaduni ufanye kazi kuanzia ngazi za chini hadi za juu, hivyo sasa utaratibu huo umekubaliwa na utaanza rasmi mwaka huu.

Aliwataka wahitimu wa TaSUBa kutumia nafasi hivyo ya kuomba kazi kwa  kuwa serikali imetangaza nafasi zaidi ya 500 za maofisa utamaduni wasaidizi.

Mwakilishi wa wazazi katika mahafali hayo , Angawile Sambala aliwataka wahitimu hao, kuendelea kuwa na nidhamu katika utendaji wa fani hizo kama walivyokuwa katika taasisi hiyo ili waendelea kuwa mfano bora wa kuigwa.

Jumla ya wahitimu 32 wa ngazi ya Stashada ya Sanaa na Utamaduni walitunukiwa vyeti vyao, ambao  kati  yao  watano wamefaulu katika daraja la kwanza na 20 daraja la pili la juu, wengine saba daraja la pili la chini.
Share this article :

0 comments:

Speak up your mind

Tell us what you're thinking... !

Google+ Followers

Total Pageviews

Comments

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. theNkoromo Blog: SPORTS PAGE - All Rights Reserved
Template Design by Creating Website Published by Mas Template