Headlines News :
Home » » KUZIONA YANGA NA SIMBA SH. 5,000 TU

KUZIONA YANGA NA SIMBA SH. 5,000 TU

Written By Bashir Nkoromo on Sunday, September 30, 2012 | 7:05 AM


Kiingilio cha chini kwenye mechi ya Yanga na Simba itakayochezwa Jumatano (Oktoba 3 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kitakuwa sh. 5,000 kwa viti vya rangi ya kijani ambavyo ni 19,648 kwenye uwanja huo wenye uwezo wa kuchukua watazamaji 60,000.

Taarifa ya TFF imesema, Mechi hiyo namba 80 ya Ligi Kuu ya Vodacom itachezwa kwenye uwanja huo kuanzia saa 11 kamili jioni. Watazamaji watakaotaka kuona mechi hiyo wakiwa wameketi kwenye viti vya rangi ya bluu ambavyo ni 17,045 watalipa sh. 7,000 kwa tiketi moja.

Viingilio vingine kwenye mechi hiyo ni sh. 10,000 kwa viti vya rangi ya chungwa ambavyo viko 11,897 wakati VIP C inayochukua watazamaji 4,060 itakuwa sh. 15,000. Kwa upande wa VIP B tiketi ni sh. 20,000 na VIP A yenye watazamaji 748 tu kiingilio kitakuwa sh. 30,000.
Share this article :

0 comments:

Speak up your mind

Tell us what you're thinking... !

Total Pageviews

Comments

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. theNkoromo SPORTS - All Rights Reserved
Template Design by Creating Website Published by Mas Template