Headlines News :
Home » » WAPENZI WA MASUMBWI MNASEMAJE KUHUSU HOJA HII?

WAPENZI WA MASUMBWI MNASEMAJE KUHUSU HOJA HII?

Written By Bashir Nkoromo on Wednesday, September 26, 2012 | 5:04 AM

KIDUNDA BAADA YA PAMBANO LAKE LA OLYMPIC UINGEREZA
Kitendo cha BFT kutokuwa na medali katika mashindano ya taifa ya ngumi ni kuonesha wazi ukata  uliokuwepo katika michezo  ya ngumi za radhaa hapa nchini.

Hii inaonesha wazi jinsi gani ngumi zinahitaji msaada wa kuyaendesha mashindano mbalimbali yanayofanyika nchini ambayo ndiyo yanayotoa wawakilishi katika mashindano ya kimataifa.

Tunajua fika kama ngumi na riadhaa ndio michezo inayojitahidi kufikia viwango vya mashindano makubwa ya kimataifa kwa wanamichezo wenyewe kujituma hivyohivyo katika mazingira yao  magumu na umaskini walionao-(tukumbuke wengi wanaocheza michezo hii wanatoka katika familia za chini kimaisha,sio cha kustaajabu mabondia wetu kula kwa mamantilie).

Na umaskini huuhuuu ndio wanaokwenda nje kupeperusha bendera,na wanapocheza tunafurahi kuwaangalia na kuwashabikia lakini hatutaki kujua maandalizi yao yapoje mpaka matokeo yawe kinyume na matarajio.

TUNAWAOMBA WADHAMINI NA WAFADHILI MJITOKEZE PIA KATIKA NGUMI hii itasaidia kuongeza hamasa zaidi kimichezo,tutakuwa na uhakika wa medali commonwealth na Olympic ,tutaongeza mikanda mingine mingi ya ubingwa wa dunia na kipato kitaongezeka kwa kodi za mabingwa  na pia nchi itatangazika vema katika Utalii, hivyo kama kuna tatizo lililobaki katika ngumi kwa wafadhili ni vizuri kuwekwa wazi likatatuliwa tukawaacha vijana wanafanya kazi.

Kwa mapungufu yaliyojitokeza katika mashindano ya taifa ya ngumi za ridhaa,BFT imeyaona kupitia katibu mkuu wake Makore Mashaga ambae alikuwa akihangaika huku na kule kuhakikisha mashindano yanafanikiwa katika mazingira yoyote,mapungufu watayafanyia kazi na pia wengine wanaostahili kupongezwa ni rais wa ngumi za kulipwa TPBO bw Yasin abdalah'ustadh kwa kutoa zawadi na hamasa kwa wachezaji na viongozi wa klabu shiriki akishirikiana na Onesmo Ngowi.

Viongozi hawa wa ngumi za kulipwa walikuwa karibu kuwasaidia wenzao wa ngumi za ridhaa kuyaendesha vema mashindano hayo ambayo ndio msingi mzuri wa ngumi za kulipwa na kweli vipaji vimeonekana mabondia walionesha ushindani wa hali ya juu,hivyo wadau wapenda maendeleo ya michezo na serikali yenyewe ni vema

Share this article :

0 comments:

Speak up your mind

Tell us what you're thinking... !

Google+ Followers

Total Pageviews

Comments

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. theNkoromo Blog: SPORTS PAGE - All Rights Reserved
Template Design by Creating Website Published by Mas Template