Headlines News :
Home » » MECHI ZA SUPER WEEKEND KUANZA KESHO

MECHI ZA SUPER WEEKEND KUANZA KESHO

Written By Bashir Nkoromo on Thursday, September 27, 2012 | 8:46 AM


NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM, TANZANIA
Michuano ya Ligi Kuu ya Vodacom inaingia raundi ya nne kesho (Septemba 28 mwaka huu) kwa mechi za Super Weekend ambazo zitaoneshwa moja kwa moja (live) na kituo cha televisheni cha SuperSport cha Afrika Kusini.

Mechi ya kwanza ambayo itachezwa kesho itakuwa kati ya Azam na JKT Ruvu Stars. Mechi hiyo itakayofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam itaanza saa 1 kamili usiku kwa viingilio vya sh. 3,000 mzunguko, sh. 5,000 kwa VIP C na VIP B wakati VIP A kiingilio kitakuwa sh. 10,000.

Jumamosi (Septemba 29 mwaka huu) kutakuwa na mechi kati ya Simba na Tanzania Prisons itakayofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 11 kamili jioni. Yanga na African Lyon zitapambana Jumapili (Septemba 30 mwaka huu kwenye uwanja huo huo kuanzia saa 11 kamili jioni.

Uwanja wa Azam Complex ulioko Chamazi, Dar es Salaam wenyewe utakuwa mwenyeji wa mechi kati ya Ruvu Shooting na Mtibwa Sugar itakayochezwa Oktoba 1 mwaka huu kuanza saa 10.30 jioni. Mechi ya mwisho ya Super Weekend itachezwa Oktoba 3 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ikizikutanisha Yanga na Simba kuanzia saa 1 kamili usiku.

RAMBIRAMBI MSIBA WA ERASTO ZAMBI
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepokea kwa masikitiko taarifa za kifo cha Katibu Mkuu mstaafu wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC), Erasto Zambi kilichotokea jana (Septemba 26 mwaka huu) jijini Dar es Salaam kutokana na maradhi.

Zambi ambaye anatarajiwa kuzikwa Jumapili (Septemba 30 mwaka huu) kabla ya kuwa kiongozi TOC, kwa muda mrefu alikuwa mwalimu wa michezo katik Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) ambapo wanamichezo wengi hasa waliokuwa wanafunzi katika chuo hicho wamepita kwake.

Msiba huo ambao uko nyumbani kwake Ubungo Kibangu, Dar es Salaam ni pigo kwa familia ya Zambi, TFF na wanamichezo kwa ujumla nchini kutokana na mchango na mawazo aliyotoa kwa shirikisho wakati akiwa kiongozi wa TOC.

TFF inatoa pole kwa familia ya Zambi, jamaa na marafiki na kuwataka kuwa na uvumilivu katika kipindi hiki cha msiba huo mzito. Mungu aiweke roho ya marehemu Zambi mahali pema peponi. Amina

Share this article :

0 comments:

Speak up your mind

Tell us what you're thinking... !

Total Pageviews

Comments

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. theNkoromo SPORTS - All Rights Reserved
Template Design by Creating Website Published by Mas Template