Headlines News :
Home » » MSIMU MPYA WA LIGI KUANZA KESHO, SEPTEMBA 15, 2012

MSIMU MPYA WA LIGI KUANZA KESHO, SEPTEMBA 15, 2012

Written By Bashir Nkoromo on Friday, September 14, 2012 | 10:51 AM


DAR ES SALAAM, TANZANIA
MSIMU mpya wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara wa 2012/13 unaanza rasmi kutimua vumbi kesho Septemba 15, ambapo timu zote 14 zitakuwa kwenye viwanja saba tofauti nchini kuwania pointi muhimu, hii ni kwa mujibu wa Ofisa Habari wa TFF Boniface Wambura.

Wambura amesema kuwa, mabingwa watetezi Simba wataikaribisha African Lyon kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, huku mjini Morogoro, Polisi Moro watakuwa wenyeji wa Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Jamhuri, wakati jijini Tanga, Mgambo JKT iliyopanda daraja itaumana na Coastal Union kwenye Uwanja wa Mkwakwani.

Tanzania Prisons ambayo nayo imerejea VPL msimu huu, itawaalika Mabingwa wa Kombe la Kagame, Yanga kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya, wakati JKT Ruvu na Ruvu Shooting zitapambana kwenye Uwanja wa Chamazi 'Azam Complex' jijini Dar es Salaam.
Azam itawatembelea Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Katiba, wakati kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza, wenyeji Toto Africans, wataumana na Oljoro JKT, ambapo mechi zote zitaanza saa 10.30 alasiri kwa saa za Afrika Mashariki.

Viingilio katika mechi ya Simba na African Lyon vitakuwa sh. 5,000 kwa viti vya rangi ya kijani na bluu, sh. 8,000 viti vya rangi ya chungwa, sh. 15,000 viti vya VIP C na B wakati VIP A itakuwa sh. 20,000. Viingilio kwa mechi nyingine vitakuwa sh. 3,000 na sh. 10,000.
Share this article :

0 comments:

Speak up your mind

Tell us what you're thinking... !

Total Pageviews

Comments

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. theNkoromo SPORTS - All Rights Reserved
Template Design by Creating Website Published by Mas Template