Headlines News :
Home » » REDDS MISS KIGAMBONI AWATOTOA KIMASOMASO KWA KUTWA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA TEMEKE

REDDS MISS KIGAMBONI AWATOTOA KIMASOMASO KWA KUTWA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA TEMEKE

Written By Bashir Nkoromo on Saturday, September 22, 2012 | 5:37 AM

Redds miss Kanda ya Temeke, Dar es Salaam,  Edda Sylivester, akiwa na mshindi wa pili Catherine Masumbigana (kushoto) na Flaviana Maeda (kulia)mara alipotangazwa kuwa Redds Miss Kanda ya Temeke kwenye fainali iliyofanyika  ukumbi wa PTA, usiku wa kuamkia Leo (Picha zote kwa Hisani ya Intellectuals Communications Limited)

BAHARI KAMILI


Edda Sylvester ndiye mshindi wa Redd's Miss Temeke 2012, katika shindano lililofanyika usiku wa kuamkia leo kwenye Ukumbi wa PTA (Sabasaba).



Licha ya kushinda taji hilo Edda amepata nafasi ya kuingia katika kambi ya Redd's Miss Tanzania na kujinyakulia kitita cha sh.milioni 1 na zawadi zenye thamaini yashilingi 500,000.

Edda ambaye ametokea katika shindano la kitongoji cha Kigamboni ataungana na Flaviana Maeda kutoka Kurasini ambaye amenyakuwa nafasi ya pili na kujichukulia kitita cha shilingi 800,000.

Mrembo Catherine Masumbigana amechukua mshindi wa tatu katika shindano hilo na kujinyakulia kitita cha shilingi 700,000.

Warembo hao watatu wamepata nafasi ya kuingia katika kambi ya Redd's Miss Tanzania ambayo itashirikisha warembo 30 ambao watakaa kambini kwa muda wa mwezi mmoja.

Warembo Jesca Haule ambaye alishika nafasi ya nne amejipatia kitita cha shilingi 400,000 na nafasi ya tano ilienda kwa Agnes Gudluck ambae amejipatia shilingi 300,000.

Washindi wote watatu kila mmoja atajipatia nguo ya kutokea jioni sanjari na viatu, vikiwa na thamani ya kila mmoja shilingi 500,000 kutoka katika Duka la kisasa la Mariedo Boutique itatoa gauni la Sh.350,000 na kiatu cha Sh 150,000 
kila mmoja kwa washindi hao watatu wa kwanza watakaoshinda. 

Warembo wengine ambao walishiriki kutoka katika vitongoji vya Kurasini,Kigamboni na Chang'ombe ambao ambao wameambualiwa kifuta jasho cha shilingi 200,000 kila mmoja ni Angela Gasper, Khadija Kombo, Neema Doreen, Flora Kazungu, Lilian Joseph, Elizabeth Peter, Elizabeth Boniphace, Zulfa Bundala, Mariam Ntakisivya na Esther Albert.

Katika shindano hilo washehereshaji walikuwa wasanii wanaong’ara katika luninga, Mpoki wa kundi la Komed Original na Steve Nyerere ambao walionekana kuvunja mbavu za mashabiki waliyoudhulia shindano hilo.

Licha ya kuwepo kwa Mpoki na Steven Nyerere Bendi ya muziki Mashujaa Wanakibega ambao waliweza kutoa burudani ya nguvu chini ya Rais wao Charles Baba.

Taji la Redd's Miss Temeke, linashikiliwa na mrembo Husna Twalib. Warembo wa Miss Temeke wamekuwa wakijifua kwa wiki tatu sasa chini ya ukufunzi wa Leyla Bhanji, ambaye amekuwa akisaidiwa pia na warembo wa miaka ya nyuma wa Miss Temeke akiwemo, Regina Mosha(20020, Hawa Ismail(2003), washiriki wa mwaka jana Joyce Maweda, Mwajabu Juma, Cynthia Kimasha na katika shoo wamekuwa na Dickson Daud kutoka kundi la THT.

Mbali ya Redd's, Miss Temeke 2012 pia imedhaminiwa na City Sports Lounge, Jambo Leo, Mariedo Boutique, Global Publishers, Dodoma Wine, Push Mobile, Mariedo Boutique, 100.5 Times FM, Kitwe General Traders, Fredito Entertainment, katejoshy.blogsport.com na 88.4 Cloud's FM. 

Temeke imewahi kutwaa taji la Miss Tanzania mara tatu, kupitia warembo Happiness Sosthenes Magesse aka Millen mwaka 2001, Sylvia Remmy Baham mwaka 2003 na Genevieve Mpangala. Lakini pia imetoa warembo waliowahi 
kushika nafasi ya pili na tano bora katika Miss Tanzania kama Jokate Mwegelo, Irene Uwoya, Irene Kiwia, Queen David, Cecylia Assey, Sabrina Slim, Miriam Odemba, Ediltruda Kalikawe na Asela Magaka.

Share this article :

0 comments:

Speak up your mind

Tell us what you're thinking... !

Total Pageviews

Comments

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. theNkoromo SPORTS - All Rights Reserved
Template Design by Creating Website Published by Mas Template