Headlines News :
Home » » YANGA YAJIKOSHA, YAITANDIKA 4-1 JKT RUVU

YANGA YAJIKOSHA, YAITANDIKA 4-1 JKT RUVU

Written By Bashir Nkoromo on Saturday, September 22, 2012 | 9:43 AM


Mshambuliaji wa Yanga Haruna Niyonzima akipambana na Sostenes Manyasi wa JKT Ruvu katika mechi hiyo. 
    Yanga ikiwa na kocha wake msaidizi  Fred Felix Minziro, leo imerejesha matumaini ya mashabiki wake, baada ya kufanikiwa kupata ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya JKT Ruvu  katika mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, iliyopigwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.


Ushindi huo umeonekana kuwapoza mashabiki machungu waliyopata baada ya timu hiyo kupigwa tatu bila mjini Morogoro, wiki iliyopita.

Katika dakika kumi za mwisho wapenzi wa yanga walijikuta wakiomba mchezo umalizike baada ya jkt ruvu kucheza mchezo mkali. Wapenzi wa simba walionekana kushangilia hali hiyo ambayo hata hivyo matokeo yakawa 4-1. 

Katika mchezo wa chamazi azam imeibuka na ushindi wa bao 1-0. Bao la azam limepatikana dakika ya 26 ya mchezo kupitia kwa  Kipre Tchetche, huku Cledo Mwaipopo akiipatia JKT Ruvu bao moja baada ya kazi nzuri ya Omar Changa na Sospeter Manyasi.

Yanga imepata bao la nne kupitia kwa Didier Kavumbangu baada ya kipa jkt ruvu kuutema mpira.
 dakika ya 52 Simon Msuva aliipatia yanga bao la tatu baada ya kuambaa ambaaa na mpira na kupachika wavuni. mapumziko Yanga imetoka kifua mbele kwa ushindi wa mabao 2-0.

 Bao la kwanza limepatikana dakika ya 4 ya mchezo kupitia kwa nadir haroub canavaro' baada ya kazi nzuri ya haruna niyonzima na Athuman Idd  Chuji dakika 31 Yanga ilipata bao la pili kupitia kwa Kavumbagu akimalizia Chuji. 

Katika kipindi cha kwanza Yanga iliweza kutawala mchezo kwa kufanya mashambulizi mengi katika lango la JKT Ruvu ambayo ilikuwa ikitumia wachezaji wake Manyasi na  Changa ambao walishindwa kufanya makeke makali hivyo mipira mingi kutoka nje.
Share this article :

0 comments:

Speak up your mind

Tell us what you're thinking... !

Total Pageviews

Comments

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. theNkoromo SPORTS - All Rights Reserved
Template Design by Creating Website Published by Mas Template