Headlines News :
Home » » COASTAL UNION YAMTAMBULISHA RAMSI M-BRAZIL WAKE

COASTAL UNION YAMTAMBULISHA RAMSI M-BRAZIL WAKE

Written By Bashir Nkoromo on Sunday, October 21, 2012 | 10:38 AM


Deangelis Gabriel Barbosa 

TANGA, TANZANIA
KLABU ya soka ya Coastal Union ya Tanga leo imemtambulisha rasmi mchezaji wake  raia wa Brazil aliyekuwa akisubiriwa kwa hamu na timu hiyo, Deangelis Gabriel Barbosa (27).
.
Mchezaji huyo Barbosa aliwasili jana jumamosi jijini Tanga akiwa na mkewe Zaira Caroline na mtoto wao Lara Barbosa ambao pia walitambulishwa katika hafla iliyofanyika leo  makao makuu ya klabu ya Coastal
yaliyopo barabara ya 12 .

Mchezaji huyo ambaye ni mzaliwa wa mtaa wa Bahia jiji la Paulo Afonso, Brazil amesema anacheza namba nane nafasi ya kiungo-mshambuliaji ambayo inahaitajika sana katika timu ya Coastal Union na kwamba amefurahi kutua kwenye timu hiyo na Tanga kwa jumla kwa kuwa hatua hiyo imemfanya kufika Tanzania na Afrika kwa mara ya kwanza.

Ameahidi kukipiga vilivyo ili kuonyesha shukurani ya aina ya mapokezi aliyopewa alipowasili jana

Kwa upande wake, Makamu Mwenyekiti wa Coastal Union,Steven Mnguto alisema tayari klabu yake ipo katika hatua za mwisho za kukamilisha kibali cha kumuwezesha kuchezea Coastal Union.

Mnguto alisema kwamba mikakati hiyo ya upatikanaji wa kibali imeshaanza na inategemewa kukamilika wiki hii na mara ya kukamilika mchezaji huyo atashuka dimbani kuitetea klabu hiyo na kwamba chezaji Barbosa amesaini mkataba wa mwaka mmoja na  wataweza  kuongeza baadae baada ya kuona ufanisi wake katika timu hiyo.

Barbosa ametokea timu ya New Road ya  Nepal ambako alijunga mwaka 2010 ambapo klabu nyingine alizowahi kuchezea ni Paham Footbal Club, Flamengo,Santa Cruz zote za Brazil na Churchill Brothers ya India ,Maruinense pamoja na Sport Club ya Jiji la Paulo Afonso.

Share this article :

0 comments:

Speak up your mind

Tell us what you're thinking... !

Google+ Followers

Total Pageviews

Comments

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. theNkoromo Blog: SPORTS PAGE - All Rights Reserved
Template Design by Creating Website Published by Mas Template