Headlines News :
Home » » IBF YAWAHAMASISHA WATANZANIA KWENDA UJERUMANI KUMSHANGILIA BONDIA CHEKA

IBF YAWAHAMASISHA WATANZANIA KWENDA UJERUMANI KUMSHANGILIA BONDIA CHEKA

Written By Bashir Nkoromo on Monday, October 22, 2012 | 10:03 AM

Cheka

NA MWANDISHI WETU
Shirikisho la Ngumi la Kimataifa (IBF) katika bara la Afrika, Mashariki ya Kati, Ghuba ya Uarabu na Uajemi linawahamasisha Watanzania wajitokeze kwa wingi kwenda kumshangilia Francis Cheka katika mpambano wake na Benjamin Simon wa Ujerumani.

Mpambamo huo ambao utafanyika tarehe 18 November 2012 katika ukumbi wa Universal jijini Berlin nchini Ujerumani utawakutanisha miamba miwili iliyosheheni kila aina ya ujuzi wa kupigana.

Watanzania wawe na tabia ya kuwaenzi wenzao wanapowakilisha taifa hili kama wenzetu wa nchi nyingine kama Kenya na Uganda wanavyofanya.

Mbali na watanzania watakaokwenda wakifuatana na Francis Cheka tokea nyumbani, pia watanzania wanaoishi nchini Ujerumani na nchi nyingine za Ulaya kama Uingereza, nchi za Skandinavia, Ufaransa, Uholanzi, Hungary na nyingine wanaombwa kujitokeza kwa wingi ili waweze kumshangilia Mtanzania mwezao aweze kupeperusha bendera ya nchi yetu vizuri.

Tayari mtangazaji maarufu wa ITV na Radio One “Maulid Baraka wa Kitenge” pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Jambo Concept inayomiliki magazeti ya Jambo Leo, City Sports Lounge, Jambo Magazine Brand Tanzania bwana Juma Abbas Pinto aliye pia mjumbe wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) wameshaonyesha nia ya kwenda Ujerumani kulitangaza pambano hilo kwenye vyombo vyao vya habari pamoja na kumshangilia Francis Cheka.

Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) inahamasishwa pia itumie nafasi hii kuitangaza nchi yetu huko Ulaya kama zinavyofanya bodi nyingine kama za Kenya, Botswana, Uganda, Oman na nyinginezo zinazotumia wanamichezo wake kutangaza vivutio vya kitalii nchini mwao.


Tunaishauri Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) izitumie nafasi ambazo watanzania wanawakilisha nchi ili kutangaza vivutio vyake vya katalii”.
Share this article :

0 comments:

Speak up your mind

Tell us what you're thinking... !

Google+ Followers

Total Pageviews

Comments

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. theNkoromo Blog: SPORTS PAGE - All Rights Reserved
Template Design by Creating Website Published by Mas Template