Headlines News :
Home » » FRANCIS CHEKA KUZIPIGA BERLIN NA MJERUMANI

FRANCIS CHEKA KUZIPIGA BERLIN NA MJERUMANI

Written By Bashir Nkoromo on Sunday, October 21, 2012 | 9:25 AM


DAR ES SALAAM, TANZANIA 
Francis Cheka wa Tanzania
Mpambano unaosubiriwa kwa hamu kubwa na wadau wa ngumi nchini Tanzania na Ujerumani kati ya Francis Cheka na Benjamin Simon wa Ujerumani sasa utafanyika tarehe 18 November katika ukumbi wa Universal jijini Berlin nchini Ujerumani. 
 
Awali mpambano huo ulikuwa ufanyike tarehe 17 November jijini Berlin, Ujerumani na tayari bondia Francis Cheka ameshasaini mkataba wa kukutana na mbabe huyo wa Ujerumani anayejulikana kwa jina la “Iron Ben” kwa ajili ya ukali wa makonde yanayowasulubu wapinzania wake.

Bondia Benjamin Simon ana rekodi ya mapambano 24 ambapo amepoteza pambano moja wakati bondia Francis Cheka ana rekodi ya mapambano 33 amepoteza mapambano 6.
Benjamin Simon wa Ujerumani
 
 
Akimwandikia “Eva Rolle” wa kampuni ya “Primetime Event Management” ya Ujerumani ambaye ndiye promoter wa mpambano huo, mwenyekiti wa ubingwa wa IBF/USBA Lindsey Tucker alimfahamisha kuwa Rais wa IBF/USBA Daryl Peoples au yeye mwenyewe Lindsey Tucker watawasiliana na mama huyo kuhusu maofisa watakaosimamia mpambano huo.
 
 
Hii itakuwa mara ya kwanza kwa wababe hao kukutana kugombea mkanda wa IBF wa mabara (IBF I/C) na mpambano wao unategemnea kutoa ushindani mkubwa.

Mshindi katika mpambano huo ataingia moja kwa moja katika orodha ya mabondia 15 bora kwenye uzito wa Super Middle duniani.

Imetumwa na:

Onesmo Alfred McBride Ngowi
Rais
IBF Africa, Mashariki ya Kati, Ghuba ya Uarabu na Uajemi
(IBF Africa, Middle East, Arabian Gulf and Persian Gulf)
Share this article :

0 comments:

Speak up your mind

Tell us what you're thinking... !

Total Pageviews

Comments

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. theNkoromo SPORTS - All Rights Reserved
Template Design by Creating Website Published by Mas Template