Headlines News :
Home » » KUONA REDD'S MISS TANZANIA SHILINGI LAKI MOJA

KUONA REDD'S MISS TANZANIA SHILINGI LAKI MOJA

Written By Bashir Nkoromo on Wednesday, October 31, 2012 | 9:39 AM


NA MWANDISHI WETU
WAKATI zikiwa zimesalia siku mbili kabla ya Redd’s Miss Tanzania 2012 kupatikana na kila mshiriki akibaki kujiuliza nani atatwaa taji hilo, kiingilio cha kushuhudia shindano hilo kimetajwa.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Mkurugenzi wa Kampuni ya Lino  waandaaji, Hashim Lundenga, alisema kiingilio kitakuwa Sh 100,000 huku kukiwa na burudani za kufa mtu.

Mshidi atajitwalia gari pamoja na fedha taslimu Sh milioni 8, katika kinyang’anyiro hicho kinachotarajiwa kufanyika kwenye ukumbi wa hoteli ya Blue Pearl uliopo jengo la Ubungo Plaza, Dar es Salaam keshokutwa.

Lundenga alisema warembo watano wamefanikiwa kuingia hatua ya 15 Bora ya Redd’s Miss Tanzania kutokana na kushinda katika mashindano madogo.

Warembo hao ni Lucy Stephano aliyeshinda Miss Photogenic, Mary Chizi aliyetwaa taji la Miss Sports Lady, Babylove Kalala aliyeshinda Miss Talent, Magdalena Roy aliyetwaa taji la Top Model na Miss Personality, Happiness Daniel.

Lundenga alisema, burudani siku hiyo itatolewa na msanii wa muziki wa kizazi kipya, Diamond Platinum, Winfrida Josephat ‘Rachel’ pamoja na yule wa ngoma za asili, Wanne Star.

 “Tumekamilisha kila kitu, naamini atapatikana mrembo mkali zaidi ambaye atatuwakilisha vema katika mashindano ya dunia,” alisema.

Lundenga alisema, tayari tiketi zinauzwa katika vituo kadhaa ambavyo ni Regency Park Hotel, Rose Garden, Share Illusion, Mlimani City, City Sport Lounge, Giraffe Hotel, Ubungo Plaza na katika ofisi za Lino.

Shindano la Redds Miss Tanzania 2012 linadhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), kupitia kinywaji cha Redds Original.
Share this article :

0 comments:

Speak up your mind

Tell us what you're thinking... !

Google+ Followers

Total Pageviews

Comments

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. theNkoromo Blog: SPORTS PAGE - All Rights Reserved
Template Design by Creating Website Published by Mas Template