Headlines News :
Home » » KILIMANJARO STARS KUREJEA LEO MIKONO MITUPU

KILIMANJARO STARS KUREJEA LEO MIKONO MITUPU

Written By Bashir Nkoromo on Sunday, December 9, 2012 | 12:44 AM


DAR ES SALAAM, TANZANIA.
Kilimanjaro Stars iliyokuwa inashiriki michuano ya Kombe la Chalenji jijini Kampala, inarejea Dar es Salaam leo Jumapili (Desemba 9, 2012).

"Timu hiyo inatarajiwa kutua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) saa 11 jioni kwa ndege ya Precisionair", limesema Shirikisho la Soka Tanzania katika taarifa yake iliyotutumia.

Imesema, baada ya Kilimanjaro Stars na Zanzibar Heroes kumaliza kushiriki mashindano ya Kombe la Chalenji jijini Kampala, Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulsen kesho Jumatatu (Desemba 10, 2012) saa 6 kamili mchana ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) atatangaza kikosi chake kitakachoingia kambini jioni ya Desemba 12, 2012 jijini Dar es Salaam kujiandaa kwa mechi ya kirafiki dhidi ya mabingwa wa Afrika, Zambia (Chipolopolo) itakayofanyika Desemba 22, 2012 katika Uwanja wa Taifa.

Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
Share this article :

0 comments:

Speak up your mind

Tell us what you're thinking... !

Total Pageviews

Comments

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. theNkoromo SPORTS - All Rights Reserved
Template Design by Creating Website Published by Mas Template