Headlines News :
Home » » RAY C APONA, AMSHUKURU RAIS KIKWETE

RAY C APONA, AMSHUKURU RAIS KIKWETE

Written By Bashir Nkoromo on Monday, December 10, 2012 | 8:43 AMMsanii wa muziki wa kizazi kipya aliyewahi kuwa nyota hapa nchini, Rehema Chalamila, maarufu kwa jina la  'RAY C',   leo amefika Ikulu jijini Dar es Salaam, kumshukuru Dk.Jakaya Mrisho Kikwete, kumshukuru kwa msaada wa matibabu aliopatiwa wakati alipokuwa mgonjwa hivi karibuni. Rehema aliyefuatana na Mama yake Mzazi Margareth Mtweve na Dada yake Sarah Mtweve alimweleza Rais kuwa afya yake imeimarika na kwamba muda si mrefu atarejea jukwaani kukonga nyoyo za mashabiki wake. Kwa apande wake ,Mama Mzazi wa Ray C amemshukuru Rais Kikwete kwa kuokoa maisha ya mwanaye na vilevile ametoa wito kwa watu wanaokusanya michango kwa ajili ya mwanaye waache kufanya hivyo kwani matibabu ya Ray  C yamegharamiwa na Rais. Pichani, akiwa na Rais Kikwete baada ya kuwasili Ikulu .
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa pamoja na Ray C, Mama mzazi RayC Margareth Mtweve (kushoto) na  dada wa Ray C Sarah Mtweve (kulia)- Picha na Freddy Maro
Share this article :

0 comments:

Speak up your mind

Tell us what you're thinking... !

Google+ Followers

Total Pageviews

Comments

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. theNkoromo Blog: SPORTS PAGE - All Rights Reserved
Template Design by Creating Website Published by Mas Template