Headlines News :
Home » » SASA NI ZAMU YA FREDERICK LAWSON NA ISSAC SOWAH KUONYESHANA UBABE

SASA NI ZAMU YA FREDERICK LAWSON NA ISSAC SOWAH KUONYESHANA UBABE

Written By Bashir Nkoromo on Tuesday, February 26, 2013 | 12:21 AM


Waghana Frederick Lawson na Issac Sowah wanatarajia kupanda ulingoni tarehe 8 Machi kugombea mkanda wa IBF katika bara la Afrika, Ghuba ya Uajemi na Mashariki ya Kati (IBF AMEPG)  katika uzito wa Welterwweight kwenye uwanja waAccra Sports jijini Accra, Ghana. Mabondia hao wamepangwa katika kapambanoi ya utangukizi wakati wa mpambano mkubwa wa kugombea mkanda wa dunia kati ya bondia wa Ghana na ambaye alikuwa bingwa wa dunia wa IBF katika uzito wa bantam Joseph Abgbeko na bondia Luis Melendez kutoka nchi ya Columbia iliyoko bara la Amerika ya Kusini. 
 
Wawili hao wanatoka katika maskani ya Bukom iliyoko kwenye kiunga cha Lebanon jijini Accra kinachosifika kwa kutoa mabingwa wengi wa dunia. Kuingia kwa mabondia hawa wawili kwenye mpambano huo kutatoa burdani ya aina yake kwa mashabiki wa ngumi wa Ghana pamoja na nchi nyingi za Afrika ya Magharibi.
Agbeko092907
Joseph Agbeko baada ya moja ya ushindi wake
IBF inaipa pongezi sana nchi ya Ghana iliyokuwa inaitwa Pwani ya Dhahabu au Gold Coast kwa kuonyesha nia thabiti ya kuinua vipaji vya mchezo wa ngumi na kuufanya mchezo huu kurudi nyumbani.  Ghana inasikfika sana kwa kuweza kutoa mabingwa wengi wa nguni wa zamani ambao walisifika sana kwa uwezo wao wa kurusha masumbi wakiwamo D.K. Poison, Marvelous Nana Yaw Konadu, Azumah Nelson, Ike "Bazooka" Quartey, Alfred "Cobra" Kotey na Joseph King Kong Agbeko ambaye anatarajia kuonyesha makeke yake siku hiyo ya tarehe 8 Machi.
 
 
ISSUED BY:
INTERNATIONAL BOXING FEDERATION AFRICA (IBF/AFRICA)
DAR-ES-SALAAM, TANZANIA
Share this article :

0 comments:

Speak up your mind

Tell us what you're thinking... !

Total Pageviews

Comments

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. theNkoromo SPORTS - All Rights Reserved
Template Design by Creating Website Published by Mas Template