KTB WA TASWA AMIR MHANDO |
DAR ES SALAAM, Tanzania
CHAMA
cha
Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) kinasikitika kuwajulisha
wadau kuwa bonanza la wanahabari lililopangwa kufanyika kesho viwanja
vya Sigara
(TCC) Chang’ombe sasa litafanyika viwanja vya Leaders Klabu, Kinondoni
Dar es
Salaam siku hiyo hiyo ya Aprili 6,2013.
Uamuzi huo wa
kushtukiza umefikiwa kwenye kikao cha dharura kilichofanyika jana usiku kati ya
TASWA ambao ni waandaaji na wadhamini wa bonanza hilo Kampuni ya Bia Tanzania
(TBL) kutokana na kushindwa kuafikiana baadhi ya mambo na menejimenti ya
viwanja hivyo.
Tunawaomba sana
radhi wanahabari kwa usumbufu mkubwa ambao wataupata kutokana na mabadiliko
haya, lakini tunaamini yamefanyika kwa dhamira nzuri yenye nia ya kuboresha
bonanza letu na kwa kiasi kikubwa litafana kwa asimilia 100.
Dhamira ya
TASWA ni kuona inakuwa na bonanza zuri
lisilokuwa na aina yoyote ya kwikwi, hivyo tayari tumeshamalizana na
menejimenti ya viwanja vya Leaders Klabu na kila kitu kitakuwa safi kuliko
maelezo.
Pia tunaishukuru
menejimenti ya viwanja vya Sigara kwa ushirikiano iliotupa kwa nia ya kufanya
bonanza hilo eneo lao, ingawa ndoto zetu hazikutumia, lakini tunaamini siku za
usoni tunaweza kufanya nao kazi.
Tunasisitiza lengo
la bonanza letu ambalo mgeni rasmi atakuwa Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison
Mwakyembe ni kuwaweka pamoja waandishi wote wa habari bila kujali ni wa siasa,
michezo, uchumi, afya na mambo mengine pamoja na wafanyakazi wa vyombo
mbalimbali vya habari, ili kubadilishana mawazo na kufurahi pamoja.
Awali bonanza letu
ilikuwa lifanyike Leaders Klabu, lakini tulilihamishia viwanja vya Sigara kutokana
na wadau wengi kuomba wapate nafasi ya kwenda kutazama mechi ya Kombe la
Shirikisho kati ya Azam ya Tanzania na Barrack Young Controllers ya Liberia
kesho. Hata hivyo tunaamini wahariri wa habari za michezo watajipanga vizuri
kulingana na mabadiliko hayo na hakuna litakaloharibika.
Pia katika
kuboresha bonanza hilo litakalotumbuizwa na bendi ya Extra Bongo na kundi la
taarabu la Jahazi Modern, kutafanyika mchezo wa soka kati ya wanahabari ambao
wameoa na wale ambao hawajaoa utakaofanyika baada ya michezo ya kawaida baina
ya vyombo vya habari kumalizika.
Bonanza litaanza
saa tatu asubuhi kwa washiriki kucheza michezo mbalimbali ikiwemo soka,
netiboli, wavu, kuruka kichura, aina mbalimbali za riadha, kuvuta kamba na
kucheza muziki. Bonanza litamalizika saa moja usiku.
0 comments:
Speak up your mind
Tell us what you're thinking... !