Headlines News :
Home » » TAMASHA LA MASTAA CHIPUKIZI KUKUTANISHA WASANII ZAIDI YA 320, JUMAPILI HII

TAMASHA LA MASTAA CHIPUKIZI KUKUTANISHA WASANII ZAIDI YA 320, JUMAPILI HII

Written By Bashir Nkoromo on Thursday, May 23, 2013 | 12:36 PM


 Mtandao wa Wasanii Tanzania (SHIWATA) 
                                             
TAMASHA la Mastaa chipukizi zaidi ya 320 la mwezi Mei litafanyika Jumapili 26, 2013 katika ukumbi wa Starlight Hotel kuanzia saa 4 asubuhi mpaka saa 10 jioni.

Mwenyekiti wa Shiwata, Caasim Taalib alisema maandalizi ya tamasha hilo yamekamilika  na vikundi vya sanaa vya Kaole, Splendid, Super Shine Taarab, Five Star Modern Taarab pamoja na wasanii mbalimbali wa Bongo Flava, Maigizo,Ngoma, Dansi na Sarakasi nao wamethibitisha kushiriki.

Taalib alisema wasanii wakongwe wa bongo flava walioalikwa ni Stara Thomas, Ommy G na waigizaji wakongwe wa Kaole na Splendid wataonesha umahiri wao katika fani ya sanaa Kauli Mbiu ikiwa ni Kilio cha Msanii .

Vikundi vingine vitakaonesha vipaji vyao ni Kepteni Shaibu, Tanzania Disabled, Uyoga Boga Village, Ndafu Arts Group, CGC, Magengistar Crew, Dodo Arts Group, Culture Arts Group, Wachapa Kazi Academy, Soweto Picture, Shiwata Commedy, Mwavionelachi, Manuari Arts Group, Tandale Morden Taarab na Begeja Wushu,

Wakati huo huo SHIWATA inawapongeza wote walioshiriki tamasha  la Aprili 27 ambako zaidi ya wasanii 300 walishiriki kuonesha vipaji.

 Pia Taalib amelipongeza Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF) kwa ushirikiano wao mzuri na kuwaomba viongozi wengine wa bendi za muziki, taarab,vikundi vya sanaa,mapromota,maprodusa na wadau wote kushiriki katika matamasha haya ili kujenga ushirikiano wa pamoja.


Peter Mwenda 
Ofisa Habari wa SHIWATA
0715/0752-222677

23/5/2013
Share this article :

0 comments:

Speak up your mind

Tell us what you're thinking... !

Total Pageviews

Comments

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. theNkoromo SPORTS - All Rights Reserved
Template Design by Creating Website Published by Mas Template