Headlines News :
Home » » JK AKUTANA NA TAIFA STARS

JK AKUTANA NA TAIFA STARS

Written By Bashir Nkoromo on Thursday, May 23, 2013 | 12:52 PM

Rais Jakaya Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Taifa Stars leo, Ikulu jijini Dar es Salaam. 

IKULU, Tanzania
Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete leo amekutana na timu ya Taifa (Taifa stars) kwa lengo la kuitia moyo katika mechi ijayo kati yake na timu ya Moroco ikiwa ni harakati za Tanzania kutafuta tiketi ya kucheza fainali za kombe la Dunia kwa mara ya kwanza  mwaka 2014.


Rais Kikwete ameiambia timu hiyo kuwa ina uwezo mkubwa  wa kusonga mbele kutokana na uwezo mkubwa waliouonesha katika mchezo wao  dhidi ya Gambia ambapo walifanikiwa kupata  ushindi wa bao 2-0.

“Maadamu mara ya kwanza mliwashinda Gambia, hakikisheni pia mnapata ushindi dhidi ya Moroco, mkishinda tunafurahi sana na mkishindwa tunanyong’onyea sana,” amesema Rais Kikwete.

Aidha amempongeza kocha wa timu hiyo Kim Poulsen  pamoja na Kamati ya Taifa ya ushindi ya Taifa stars kwa kuisaidia timu hiyo kiasi cha shilingi milioni 30 ikiwa ni mkakati wa kuiongezea nguvu kwa hatua iliyofikia  na kuwataka wachezaji kujituma ili kuwafurahisha watanzania ambao hivi sasa wanaipenda timu yao ya Taifa.

 Nae Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Fenera Mukangara amesema Serikali itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali wa michezo nchini  ili kuondoa changamoto zinazoikabili timu hiyo.

Kwa upande wake Kocha Poulsen, amemshukuru Rais Kikwete kwa kuwakaribisha na kuwatia moyo ambapo ameahidi kuifundisha vizuri timu hiyo ili kuhakikisha kuwa wanapata ushindi.

Akizungumza kwa niaba ya wachezaji wenzake kaptaini wa timu hiyo Juma Kaseja amemshukuru Rais Kikwete na kuahidi kujituma kwenye mazoezi na hatimaye kuibuka washindi  kwenye mechi zijazo.

Taifa stars ambayo inakamata nafasi ya pili katika kundi C inatarajia kucheza ugenini na Morocco mnamo Juni 7 mwaka huu.
Share this article :

0 comments:

Speak up your mind

Tell us what you're thinking... !

Total Pageviews

Comments

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. theNkoromo SPORTS - All Rights Reserved
Template Design by Creating Website Published by Mas Template