Headlines News :
Home » » BALIMI YANUFAISHA WADAU SHINYANGA KWA MASHINDANO YA NGOMA

BALIMI YANUFAISHA WADAU SHINYANGA KWA MASHINDANO YA NGOMA

Written By Bashir Nkoromo on Sunday, June 23, 2013 | 9:33 AM

Kiongozi wa kundi laNgoma la Wagoyangi, Ngelela Ng'wanajiluguja (katikati) akifurahia kitita cha shilingi laki sita mara baada ya kukabidhiwa na Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Annarose Nyamubi (wa pili kushoto) baada ya kuibuka mabingwa katika mashindano ya Ngoma Mkoa wa Shinyanga yanayodhaminiwa na Bia ya Balimi, yaliyomalizika mwishoni mwa wiki Mkoani humo. Kushoto ni Meneja Mauzo wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) Mkoa wa Shinyanga, Robert Kazinza na Meneja matukio TBL Kanda ya Ziwa, Erick Mwayela.


SHINYANGA, Tanzania.
KUNDI la Ngoma la Mwanajilunguja limefanikiwa kutwaa ubingwa wa mashindano ya Ngoma Mkoa wa Shinyanga yanayodhamniwa na Kampuni ya Bia Tanzania kupitia kinywaji Balimi Extra Lager yaliyomalizika mwishoni mwa wiki mkoani humo.

Kundi la Mwanajilunguja lilitwaa ubingwa huo kwa alama 82,na kuzawadiwa fedha taslimu Sh.600,000/= na tiketi ya kuwakilisha Mkoa wa Shinyanga katika fainali za mashindano ya Kanda yanayotarajiwa kufanyika Julai 20 mwaka huu jijini Mwanza.

Washindi wa pili katika mashindano hayo ni kundi la Mabulo ya Jeshi ambao walipata alama 80 hivyo kujinyakulia fedha taslimu Sh.500,000/=,nafasi ya tatu ilichukuliwa na kundi la Wagoyangi Usule kwa alama 79 na kuzawadiwa Sh.400,000/=,nafasi ya nne ilichukuliwa na Wagoyangi Bugimbagu kwa alama 73 ambao walizawadiwa Sh.400,000/= 

Jumla ya vikundi vilivyoshiriki mashindano ya Ngoma Mkoa wa Shinganga  ni 10,ambapo vikundi shiriki 6,vingine vilipewa kifuta jasho cha fedha taslimu Sh.150,000/= kila kikundi.

Akizungumza na washiriki wa mashindano hayo pamoja na wakazi wa Shinyanga waliojitokeza kushuhudia fainali hizo, Mkuu wa Wilaya ,Annarose Nyamubi aliwapongeza washiriki wote kwa ushiriki wao katika mashindano hayo na pia kwa kuendeleza mila na desturi za ngoma za asili lakini zaidi aliipongeza Kampuni ya Bia Tanzania kupitia Bia ya Balimi  Extra Lager ambao wanadhamini mashindano hayo kwa kujua udhamani wa Ngoma za asili.

Mkuu huyo wa wilaya amesema kuwa kwa kutumia mashindano kama hayo jamii imekuwa ikiburudika na  kutukumbusha tamaduni zetu ambazo mara nyingi zimekuwa zikisahaulika kwa wengi na kuiomba kampuni ya TBL kuendelea kudhamini mashindano hayo na kuwataka kutosita kushilikiana na serikali katika masuala mbalimbali ya kijamii kwa kuwa kwa kufanya hivyo wamekuwa wakisaidia baadhi ya majukumu ya serikali.

Aidha mkuu huyo wa wilaya amevitaka vikundi hivyo kuzitumia fedha wanazo zipata katika kujiletea maendeleo ikiwemo kuanzianzisha vikundi vya kuweka na kukopa ili viweze kuwasaidia katika kuwalete maendeleo.

Naye Meneja wa Kampuni ya bia Tanzani (TBL) Robert Kazinza amesema kuwa kampuni yake imekuwa ikishiriki katika kudhamini  shughuli mbalimbali za kijamii ikiwemo michezo na burudani ikiwa ni shukrani zao kwa jamii kwa kutumia bidhaa zao ambapo ameiomba jamii ili kampuni hiyo iweze kuendelea kudhamini shughuli hizo wawaunge mkono kwa kutumia bidhaa zao, hasa bia ya Balimi Extra Lager bia ya Kanda ya Ziwa pekee.

Vikundi vingine ambavyo vimeshiriki katika fainali hizo ni pamoja na Buzoli Ngunga, Kadete, Wagoyangi Maswa, Waulinguli Bugimbagu, Bugali na Shinyanga Art Group, fainali hizo zitaendelea wiki ijayo ili kumpata mshindi wa fainali hizo katika mkoa wa Kagera, ambaye ataungana na washindi wengine ambao watashiriki mashindano hayo ngazi ya kanda yatakayo fanyika jijini Mwanza Hivi karibuni.
Share this article :

0 comments:

Speak up your mind

Tell us what you're thinking... !

Google+ Followers

Total Pageviews

Comments

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. theNkoromo Blog: SPORTS PAGE - All Rights Reserved
Template Design by Creating Website Published by Mas Template