Headlines News :
Home » » MATUSI YA NGUONI YADAIWA KUWA SABABU YA STARS KUSHINDWA NA IVORY COAST!!!!!

MATUSI YA NGUONI YADAIWA KUWA SABABU YA STARS KUSHINDWA NA IVORY COAST!!!!!

Written By Bashir Nkoromo on Thursday, June 20, 2013 | 6:14 AM

NA BELINDA KWEKA-MAELEZO 
Wakati Watanzania hususan wapenda kandanda  wakiwa bado wanatafakari kwa machungu kipigo cha mabao 4-2, ilichopata Taifa Stars kutoka kwa Ivory Coast, wadau wengine wameibuka na madai kwamba matusi ya nguoni yanayodaiwa kuhanikizwa na mashabiki wakati wa mechi hiyo ndiyo sababu ya kipigo hicho!

Madai hayo yametolewa leo mchana kweupe na Maaskofu na Wachungaji wa Good News For All Ministry wakati wakizungumza na waandishi wa   habari leo  katika ukumbi wa mikutano wa Idara ya Habari – MAELEZO  jijini Da res Salaam.

Askofu Charles Gadi amesema kuwa kuna sababu nyingi zilizopelekea Taifa Stars kushindwa katika mchezo wake na Ivory Coast uliopigwa Juni 16, mwaka huu kwenye dimba la Taifa, jijini,  ni pamoja na matusi na mzaha unaofanywa na wananchi wenyewe.

“Ndugu waandishi, ni kweli goli la kwanza lilifungwa kwa maombi ya Watanzania waliokuwa wakiomba, lakini matusi yaliyoendelea pale uwanjani ambayo yanatukana maumbile ya mama, dada, wakwe na watoto zetu wa kike yalitukwamisha.

“ Unapotukana kwa kutumia maumbile ya wakina mama ni sawa na kuchafua,kujeli uumbaji wa Mungu kwa wakina mama. Hali hiyo hutuletea laana ya kushindwa,” alisema Askofu Gadi.

Aliongeza kuwa walianza kuiombea Taifa Stars toka mwaka 2012 ili ifanikiwe katika mechi zake zote hivyo wana uchungu kwa kufungwa na timu hiyo ya kigeni.

Aidha Askofu Gadi aliongeza kuwa pale uwanjani kulikuwa kumefurika watu wengi hivyo kuhatarisha usalama wa watu walioko pale na hivyo ameiomba  Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) litoe tiketi kulingana na idadi ya viti vilivyopo uwanjani.

Pia Askofu Gadi amesema kuwa wana maombi ya siku elfu moja kwa ajili ya kuliombea Taifa zima, mpaka sasa wamekaribia siku mia tano katika maombi  hayo hivyo wanaomba watu kutokwamisha maombi yao kwa kuacha matusi.

“Naomba Watanzania wamwogope Mungu kwa kuacha matusi na dhambi zao kwani wakifanya hivyo nchi itakuwa na maendeleo na kuwa ya kistaarabu kwa kuendeleza amani,” alisisitiza Mchungaji Leonard Kijuna.

Pia Askofu Gadi ametoa wito kwa Serikali kuwa waweze kutunga sheria kuhusu matusi kwamba endapo mtu atapatikana akitukana basi achukuliwe hatua kama zilivyo nchi njingine,mtu akitupa bigijii anafungwa, kwani  itasaidia kutokomeza kabisa suala hilo.
Share this article :

0 comments:

Speak up your mind

Tell us what you're thinking... !

Total Pageviews

Comments

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. theNkoromo SPORTS - All Rights Reserved
Template Design by Creating Website Published by Mas Template