Headlines News :
Home » » ROSEMARY PETER AVISHWA TAJI LA REDDS MISS NYAMAGANA 2013, BAADA YA MSHINDI WA TAJI HILO DIANA AMIMO KUDANGANYA URAIA NA UMRI WAKE.

ROSEMARY PETER AVISHWA TAJI LA REDDS MISS NYAMAGANA 2013, BAADA YA MSHINDI WA TAJI HILO DIANA AMIMO KUDANGANYA URAIA NA UMRI WAKE.

Written By Bashir Nkoromo on Friday, June 7, 2013 | 1:12 PM

Mkurugenzi wa Club Fusion wadhamini wa shindano la Miss Nyamagana 2013, Mr. George akipeana mkono na Redds Miss Nyamagana 2013 Rosemary Peter, mara baada ya kuvishwa taji hilo. 

>>>>>Rosemary Peter, ni mshindi wa pili katika shindano la kumtafuta Redds Miss Nyamagana 2013, shindano lililofanyika tarehe 11/05/2013 katika ukumbi wa JB Belmont Hotel jijini Mwanza.

Alhamisi ya tarehe 06/06/2013, Rosemary peter amevishwa taji la Redds Miss Nyamagana 2013, baada ya Diana Amimo aliyekuwa mshindi wa taji hilo kudaganya Uraia na umri wake katika shindano hilo.

Udanganyifu huo uligunduliwa na kuthibitishwa na idara ya uhamiaji mkoa wa Mwanza, baada ya maafisa wake kumshikilia na kumuhoji mrembo huyo, wiki moja mara baada ya shindano hilo.

Kwa Mujibu wa kanuni na vigezo vya mashindano ya urembo hapa nchini, kuwa Msichana lazima awe raia wa Tanzania na mwenye umri wa miaka 18 hadi 24, Kampuni ya Stoppers Entertainment, imeweza kumvua taji mrembo Diana Amimo na kumvisha mshindi wa Pili Rosemary Peter kuwa Redds Miss Nyamagana 2013/14
Share this article :

0 comments:

Speak up your mind

Tell us what you're thinking... !

Total Pageviews

Comments

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. theNkoromo SPORTS - All Rights Reserved
Template Design by Creating Website Published by Mas Template